Tuesday, June 4, 2013

Thursday, May 23, 2013

MTWARA : GESI GESI WAR UPDATE

  • Kuna madai ambayo hayajathibitishwa kwamba wanawake wanabakwa na maaskari, wanapigwa risasi kutokana na vijana wote kukimbia maporini.
  • Mwanamke anayekadiriwa miaka 25 mjamzito auawa kwa kupigwa risasi maiti ipo Ligula.
  •  Mwanafunzi wa CHUNO afikishwa hospitali  Ligula na majeraha ya risasi mguuni.
  • Maduka maeneo ya Magomeni yamechomwa moto ikiwamo pia mali za Askari magereza na uhalifu ukifanyika vidole vinawaelekea Polisi.
  • Afisa Usalama wa Taifa ambaye anamiliki nyumba ya wageni naye amevamiwa na kuporwa mali ikiwamo fedha katika gesti yake. Haijajulikana ni kiasi gani cha mali kilichopotea.
  • Mabomu yanaendelea kupigwa tofauti kwa sasa hayapigw mfululizo.
  •  Mabomu yametulia. Hali ya ukimya imetawala.
  • Mabasi 5 ya Champion yamebeba Wanajeshi yako njiani yanakuja.
  •  Serikali yatoa tamko yasema watu 91 wanashikiliwa.
  • Bunge laahirishwa tena. Kupisha uchunguzi na kuepusha uchochezi kutoka kwa baadhi ya wabunge. (Kwa mujibu wa Spika)
  •  Maeneo ya Magomeni, Chikongola, Nkanaledi, Mikindani  maaskari wanaingia majumbani mwa watu na kumsomba mtu yeyote ambaye ni mwanaume awe amehusika awe hajahusika na kumkamata. Pia inaripotiwa na uhalifu unafanywa na maaskari hao hao.  Jambo linaloamsha hisia kwa wananchi.
  • RPC anaongea na vyombo vya habari na kuwasihi wananchi waende makazini. Lakini kiuhalisia hali sio shwari.
  • Mahakama ya mwanzo ya Mitengo imechomwa moto
  • Mpaka sasa ni vita baina ya wananchi na maaskari. Mabomu yamesikika pamoja na milio ya risasi masaa 24. Na milio ya Risasi na mabomu inaendelea kusikika.
  • Raia wapatao 7 wameripotiwa kufariki (wengine walipelekwa hospitali ya Ndanda Ndogo na mmoja ameripotiwa kupokelewa Ligula.
  • Nyumba za viongozi zinaendelea kuchomwa moto.
  • Majibizano baina ya Polisi na Raia yanaendelea maeneo ya Magomeni, Nkanaledi na Mikindani.

  • Maduka yamefungwa na hakuna huduma zozote
      Barabara zimewekwa vizuizi magogo na matairi yamechomwa moto. Hakuna njia ya kupita.  

      MTWARA LEO




      PICHA NA FARID HEMED




         SHUJAA WA GESI ALIYEPIGWA RISASI 
         RIP Kaka Karim(Picha Mpasta, JAMII FORUMS)

        Monday, May 13, 2013

        Polisi Yabaini Bomu Lililorushwa Kanisani Arusha ni la Kiwandani


        Kamanda wa Polisi Arusha, Lebaratus Sabas

        SIKU saba baada ya tukio la mlipuko wa bomu katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi,Olasiti mkoani Arusha, Jeshi la Polisi limesema kuwa mlipuko huo ulitokana na bomu lililotengenezwa kiwandani.
        Taarifa hiyo ni sehemu ya matokeo ya uchunguzi unaofanywa kutokana na tukio hilo lililotokea Jumapili iliyopita, kupoteza maisha ya watu watatu na kujeruhi wengine 67 baadhi wakiwa katika hali mbaya.
        Polisi nchini kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola na Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) vipo katika uchunguzi kuhusu tukio hilo lililotokea muda mfupi kabla ya kanisa hilo kuzinduliwa rasmi ambapo mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Vatican nchini Askofu Mkuu Francisco Padilla.
        Akizungumza na gazeti hili jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Lebaratus Sabas alisema kuwa uchunguzi umebaini kuwa bomu hilo siyo la kutengenezwa kienyeji, bali ni la kiwandani.
        “Uchunguzi wa awali unaonyesha, bomu lililotupwa kanisani siyo la kutengeneza kienyeji. Hii ni kwa mujibu wa taarifa tulizozipata kutoka kwa wataalamu ndani ya Jeshi la Polisi,” alisema na kuongeza:
        “Taarifa kamili itatolewa Jumatatu (kesho) kwa kuwa kuna baadhi ya watuhumiwa wanaendelea kukamatwa na kuhojiwa na polisi na wengine watafikishwa mahakamani.”
        Kamanda Sabas alisisitiza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na halitasita kutoa taarifa kwa umma kukiwa na haja ya kufanya hivyo, ambapo amewaomba wote wenye taarifa zinazoweza kusaidia upelelezi kuzitoa polisi.
        Arusha na Ugaidi
        Taarifa hizo zimekuja huku mji wa Arusha ukianza kuingia katika rekodi mbaya ya kuhusishwa na vitendo vya ugaidi, baada ya matukio matatu kuuhusisha mji huo wa kitalii nchini.
        Kuhusishwa kwa mji huo na ugaidi kunatokana na wahusika wakuu wa milipuko iliyotokea nchini na nchi jirani kudaiwa kwamba waliratibu vitendo hivyo wakiwa katika mji huo.
        Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa mwaka 1998 mtuhumiwa mkubwa wa ugaidi, Ahmed Khalfan Ghailani, alidaiwa kukaa kwa muda mjini Arusha na kununua baruti za kulipulia miamba kutoka kwa baadhi ya wachimbaji wa madini ya Tanzanite Mirerani, Wilaya ya Simanjiro.
        Baadaye ilibainika kuwa mabomu yaliyotumika kulipua Ofisi za Ubalozi wa Marekani katika miji ya Dar es Salaam na Nairobi nchini Kenya katika tukio la Agosti 7, mwaka huo wa 1998, malighafi zake zilinunuliwa mkoani Arusha na Ghailani.
        Katika tukio jingine la mwaka 2011, wakazi wawili wa Arusha, Abdulmalik Majid na Hija Seleman Nyandondo (30), walikamatwa kwa tuhuma za kushiriki njama za kuilipua kwa bomu klabu moja ya usiku katika Jiji la Kampala nchini Uganda lililopoteza maisha ya watu 74, waliokuwa wakitazama mpira wa Fainali za Kombe la Dunia, mwaka 2010.
        CHANZO: Mwananchi

        Tuesday, May 7, 2013


        kitambi 8f698
        The DVD & Audio CD "Kupunguza Unene Na Kitambi" is now available and will soon be launched. This is a joint Project between ConsNet Group and The Eastern Africa Professionals & Business Network - EAPBN.
        In this DVD; Losing Weight and Big Belly is a matter of mathematics. You need to know what are the HIGHEST THERMIC EFFECT FOODS. Simply these are foods which when you take: The digestive, absorption and other processes takes a lot of Calories out of your body than what calories is brought in by these foods.
        The net effect is lot of fats can be burnt faster than working hard on GYMS. However exercises are also very important.Our recorded Talks comes in various topics ranging from Health; Success; Entrepreneurship; Leadership; Women Affairs; Sales & Marketing etc. and will be available regularly.
        We have speakers from Tanzania & various Eastern African countries.All our our series are addressing 4 key issues:
        1. The Problem at hand
        2. Cause of the problem and its effects
        3. Solution to the problem
        4. Motivation to encourage someone to change and take action.

        If you are interested to be a Distributor, you need to buy more than 100 copies at TZS 3,000 per copy. You will sell at TZS 5,000. Serious inquiry can contact as via provided contacts in the poster.
        Sanctus Mtsimbe

        Mlipuko Arusha; Wasaudia Wanne Mbaroni, FBI Watua Arusha


        Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal akimjulia hali Restuta Alex (50), aliyelazwa katika Hospitali ya Mount Meru Arusha, baada ya kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu uliotokea juzi. Kushoto ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa na Kulia ni Mkurugenzi wa Maelezo, Assah Mwambene. Picha ya OMR 
        WAKATI maofisa wa Shirika la Upelelezi wa Marekani (FBI) wametua Arusha, raia wanne wa Saudi Arabia na Watanzania wawili wamekamatwa kwa tuhuma za kuhusika kulipua bomu lililoua watu wawili na kujeruhi wengine 61 wakati wa ufunguzi wa Kanisa la Mtakatifu Joseph Parokia ya Olasiti.
        Waliofariki dunia ni Regina Longino Kurusei (45), mkazi wa Olasiti na James Gabriel (16), ambaye alifariki usiku wa kuamkia jana. Tukio hilo lilitokea wakati Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa nchini, Francisco Montecillo Padilla alipokuwa akizindua kanisa hilo.
        Akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo alisema raia hao wa Saudi Arabia walikamatwa jana asubuhi baada ya tukio wakiwa kwenye gari wakielekea Kenya kupitia Namanga. Mulongo alisema raia hao wa kigeni waliingia nchini Jumamosi iliyopita na siku iliyofuata ndipo kukatokea ulipuaji huo. Alisema lengo la shambulizi hilo lilikuwa kumdhuru Askofu Padilla.
        “Mtu ambaye tulimkamata jana (juzi Jumapili) ndiye aliyesaidia kuwapata watu hawa wa Saudi Arabia na Watanzania hao,” alisema Mulongo.
        Mulongo alisema maofisa wa FBI walifika jana saa tano asubuhi ili kusaidiana na Polisi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), katika uchunguzi wa tukio hilo. Maofisa hao wa FBI walikuwa Zanzibar ambako walikuwa wanachunguza kifo cha Padri Evaristus Mushi ambaye aliuawa Februari 17, mwaka huu.
        Hii itakuwa mara ya pili kwa wageni kuhusishwa na matukio ya ugaidi nchini baada ya mwaka 1998 wakati raia kadhaa wa Misri wakiongozwa Fazul Abdulla waliposhirikiana na Watanzania kadhaa akiwamo Ahmed Ghailani kulipua ubalozi wa Marekani nchini na ule wa Kenya. Ghailani anatumikia kifungo cha maisha nchini Marekani wakati Fazul aliuawa Somalia mwaka 2011.
        Tamko la Serikali
        Akitoa tamko la Serikali bungeni jana, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alimtaja mmoja wa watuhumiwa wanaoshikiliwa kuhusika na tukio hilo kuwa ni Victor Calisti Ambrose (20), mkazi wa Kwa Mrombo Arusha ambaye ni dereva wa bodaboda. Alisema kijana huyo ndiye anayetuhumiwa kurusha bomu hilo.
        Waziri Nchimbi alitoa onyo kali kwa wanasiasa wanaopandikiza chuki za kidini miongoni mwa Watanzania na kuishutumu Serikali kutokana na matukio kama hayo. “Kuna wanasiasa ambao wanaona masilahi yao ni muhimu kuliko maisha ya Watanzania, masilahi yao ni muhimu kuliko utulivu wa Watanzania na masilahi yao ni muhimu kuliko umoja wa Watanzania.”
        JK akatiza ziara, Bilal atoa ahadi
        Rais Jakaya Kikwete, amekatiza ziara yake ya kiserikali nchini Kuwait ili kurejea nyumbani kutokana na shambulio la bomu kwenye kanisa hilo. Taarifa ya Ikulu imesema jana kwamba Rais Kikwete amelazimika kukatiza ziara hiyo na kurejea nyumbani mara moja ili kuwa karibu na wafiwa pamoja na wale waliojeruhiwa katika shambulio hilo la kigaidi. Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilal ameahidi kuwa Serikali itahakikisha wote waliohusika na tukio hilo wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola.
        Balozi wa Papa atoa tamko
        Askofu Padilla ambaye jana alitembelea majeruhi katika Hospitali ya Mkoa, Mount Meru, alieleza kustushwa na tukio hilo na kusema hakutarajia kitu kama hicho kutokea wakati wa shughuli hiyo wakati Watanzania wakijulikana ni watu wa amani. Alilaani tukio hilo na kuvitaka vyombo vya usalama kufanya uchunguzi ili kubaini ukweli.
        Kanisa Katoliki Arusha
        Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Arusha jana liliitaka Serikali iwataje waliohusika na tukio hilo la kigaidi huku likiwataka waumini wake kutolipiza kisasi.
        “Msimamo wa kanisa katika hili, ni kuwataka waumini wasilipize kisasi kama ambavyo alisema Yesu Kristo kuwa msilipize kisasi, muwe tayari kushinda ubaya kwa wema,” alisema Askofu Josephat Lebulu na kuongeza:
        Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU)
        Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU), imetaka kuharakishwa kwa uchunguzi wa tukio hilo na kuonya kuwa matukio kama hayo yanaweza kulitumbukiza taifa kwenye machafuko. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Balozi wa Umoja huo nchini, Filiberto Ceriani-Sebregondi alisema Tanzania inapaswa kufahamu kwamba pasipo kujenga, kuendeleza na kusisitiza utamaduni wa kuvumiliana, hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa siku za usoni

        TSH. Bilioni 876.3 Kutatua Msongamano wa Magari Dar



        Na Immaculate Makilika- Maelezo
        SERIKALI imesema   inatekeleza miradi ya kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam yenye thamani ya sh. bilioni 876.336   katika barabara ya Al Hassan Mwinyi ambapo watumiaji wa barabara hiyo hutumia takribani saa moja na nusu kufika Osterbay polisi hadi daraja la Salender hususani mida ya asubuhi saa moja hadi saa tatu.
        Hayo  yalisemwa leo Bungeni na  Naibu Waziri wa Ujenzi   Gerson  Lwenge Naibu  wakati    akijibu swali  Mbunge  wa Jimbo la  Temeke  Abasi Zuberi Mtemvu  lililouliza kuwa  Je,Serikali inaweza kutoa ufafanuzi juu ya ufumbuzi wa tatizo la msongamano huo?
        Alisema   kuwa  inayolenga kutatua tatizo hilo ,ikiwemo miradi ya kupunguza msongamano wa magari katika jiji hilo ambayo ni  kama ifuatavyo;.Barabara ya Kimara –Kivukoni (fire),Fire-Kariakoo na Magomeni –Morocco (Sh.  bilioni 240),Karakana na vituo vya mabasi yaendayo kwa haraka (BRT) pamoja na kuhamisha nguzo za umeme(sh. bilioni 47.90).
        Nyingine ni  Barabara ya Mwenge – Tegeta(sh.  bilioni 88.00),Barabara ya Kilwa (Kilwa Road) Bendera Tatu-Mbagala Rangi Tatu ,(sh.  bilioni 35.16),Daraja la Kigamboni (sh. 214.64).Flyover ya TAZARA,Serikali ya Japani imetoa msaada wa fedha kwa ajili ya usanifu,.Barabara ya Gerezani (Bendera –Tatu-KAMATA),Serikali ya Japani imetoa  msaada wa fedha kwa  ajili ya ujenzi.
        Barabara ya Mandela (sh. bilioni 61.25) na.Barabara ya  Wazo Hill –Bagamoyo-Msata (sh. bilioni 89.61).
        Waziri  huyo  alisema  ujenzi wa mabasi yaendayo haraka(BRT) kutoka Morocco kwenda Magomeni hadi Kivukoni na Kimara yatapunguza msongamano wa magari kati ya Osterbay Polisi na Daraja la Salender.
         Aliongeza kuwa katika mipango ya baadae ,Serikali itaangalia uwezekano na kujenga barabara ya juu  (viaduct) pande zote za daraja ,kujenga daraja lingine pembeni mwa daraja la Salender au kujenga njia mbadala (salender bridge Bypass) kutokea Kenyata Drive  kuunganisha na Ocean Road..

        Kauli ya BAKWATA kuhusu mlipuko uliotokea Kanisani Olasiti, Arusha


        MK/HB.VOL.6/013/1 

        06/05/2013

        TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI    

        TAMKO LA BARAZA KUU LA WAISLAMU WA TANZANIA BAKWATA JUU YA MLIPUKO WA BOMU - ARUSHA

        Assalaam alaykum warahmatullahi wabarakaatuh.
        Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania BAKWATA, limepokea kwa masikitiko makubwa tukio la kurushwa bomu Kanisani na kusababisha upotevu wa maisha na majeraha kwa watu wengi wakati wa sherehe ya uzinduzi wa jengo la Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Orasiti, Arusha.

        Kimsingi hili ni jambo la kusikitisha, kukera na kufadhaisha sana kutokea hapa nchini. Watanzania kwa miaka mingi, tumezoea hali ya utulivu na amani na tukio kama hili ni changamoto kwa usalama wa Watanzania wote nchi nzima Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania BAKWATA linalaani kitendo hicho cha kikatili na inaviomba vyombo vya dola kufanya jitihada zote kuhakikisha wahusika wanakamatwa na wanachukuliwa hatua, kwani msiba huu ni wetu sote, Wakristo na Watanzania wote.

        Kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania mimi Sheikh Issa Bin Shaaban Simba Mufti wa Tanzania nawapa pole wafiwa wote katika tukio hilo na kuwaombea dua majeruhi na Mwenyezi Mungu (SW) awape tahfif na wapone haraka na kurudi katika shughuli zao za kila siku.
        Wabillahi Tawfiiq.

        SHEIKH ISSA BIN SHAABAN SIMBA.
        MUFTI NA SHEIKH MKUU WA TANZANIA BARA

        Monday, May 6, 2013

        Tafuteni njia ya kuinusuru MSD - W/Mkuu aiagiza TAMISEMI na Naibu Waziri



         
        Picture
        Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua madawa yaliyohifadhiwa kwenye boahari ya MSD ya Kanda ya Kati eneo la Kizot mjini Dodoma baada ya kuzindua bohari hiyo Mei 5,2013. Wapili Kulia ni Naibu Waziei wa Afya, Dkt.Seif Rashid , Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD, Malima Lubeleje na wapili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
        TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

        PINDA: TAFUTENI NJIA YA KUINUSURU MSD

        WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amemwagiza Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid awasiliane na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili watafute njia ya kuinusuru Bohari ya Dawa (MSD).

        Amesema hawana budi kutafuta njia ya kuhakikisha kuwa asilimia 67 inayotengwa na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) kwa ajili ya kulipia dawa za wagonjwa mbalimbali inatumiwa ipasavyo na si vinginevyo.

        Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumapili, Mei 5, 2013) wakati akizindua ghala jipya la kisasa la kuhifadhia dawa lililojengwa na Bohari ya Dawa, Kanda ya Dodoma  huko Kizota, nje kidogo ya mji wa Dodoma.

        Ujenzi wa ghala hilo ambao umegharimu sh. bilioni 9.9/-, umechangiwa na Serikali ya Marekani kupitia Shirika lake la USAID na Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund).

        “Naibu Waziri kaeni na TAMISEMI ili itafute njia inayofaa kuzibana Halmashauri zote ili fedha inayotolewa na Mfuko wa Bima ya Afya zote ziende kutumika kwenye manunuzi ya dawa na si vinginevyo. Bima ya Afya wanataka asilimia 67 ya fedha wanayotoa itumike kulipa dawa na asilimia 33 iwe kwa matumizi mengine,” alisema.

        Alikuwa kijibu risala ya MSD iliyosema Bohari ya Dawa inaidai Serikali kiasi cha sh. bilioni 52 ambazo zimelimbikizwa kutokana na madeni ya muda mrefu ya huduma za dawa, vifaa, na vifaa tiba ambavyo taasisi hiyo ilitoa kwa vituoa vya afya vya Serikali pamoja na hospitali zake.

        Aliipongeza MSD kwamba licha ya mzigo mkubwa wa deni ilionao, haijaacha Kutoa huduma ya kununua na kusambaza kwa wananchi. Alisema Serikali itajitahidi kutafuta mbinu za kupunguza deni hilo katika bajeti ya mwaka huu.

        Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na hadahara iliyohudhuria uzinduzi huo, Dk. Seif Rashid alisema hivi sasa Bohari ya Dawa ilikuwa inakodisha mita za mraba 24,000 kwa ajili kupata nafasi ya kuhifadhia dawa zinaingizwa kutoka nje ya nchi na kwamba kukamilika kwa ujenzi wa ghala hilo, lenye mita za mraba 5,310 kutasadia kupunguza gharama hizo.

        Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa, Bw. Cosmas Mwaifwani alisema kuanzishwa kwa taasisi kumesaidia kuongeza kiwango cha upatikanaji wa dawa kutoka asilimia 44 mwaka 1994 na kufikia asilimia 70 hadi 75 hivi sasa.

        Alisema ili kuhakikisha dawa zinapatikana kwa wakati hadi vijijini, Bohari ya Dawa imeshaingiza mikoa 10 kwenye mfumo wake wa usambazaji wa dawa moja kwa moja hadi kwenye vituo vya afya badala ya kuishia kwa Mganga Mkuu wa Wilaya.

        Alisifu Halmashauri sita na hospitali moja ya mkoa kwa kuwa mfano bora kwenye usimamizi na matumizi ya dawa zinazotolewa na kusambaza na Bohari ya Dawa. Alizitaja Halmashauri hizo kuwa ni Iramba, Bariadi, Igunga, Chamwino, Bahi na Sumbawanga. Aliitaja Hospitali ya Mkoa wa Iringa kuwa ndiyo iliyofanya vizuri kuliko hospitali nyingine nchini.

        Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Dodoma, mwakilishi wa wahisani, wafanyakazi wa MSD na wakazi wa Kizota.
           
        (mwisho)

        IMETOLEWA NA:
        OFISI YA WAZIRI MKUU,
        S. L. P 980,
        DODOMA.


        Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2SVxbjaqV

        Mmoja Afariki, Majina ya Majeruhi Mlipuko Kanisa Katoliki Arusha Yatajwa


        Mmoja wa majeruhi wa mlipuko huo akihudumiwa
        Polisi wakichunguza sehemu ambayo kitu kilicholipuka kiliangukia
        Kanisa la Mt. Joseph Mfanyakazi, Olasiti Arusha (Picha zote kwa hisani ya audifacejackson.blogspot.com)
        TAARIFA za mwendelezo wa tukio la mlipuko wa kitu kinachohisiwa kuwa ni bomu katika Kanisa Katoliki la Mt. Joseph Mfanyakazi zinasema mtu mmoja tayari amefariki dunia huku zaidi ya majeruhi 30 wakiendelea kutibiwa katika hospitali mbalimbali Mkoani Hapa kufuatia mlipuko huo.
        Baadhi ya majina yaliyotajwa hadi sasa ya majeruhi ni pamoja na Vovalt John, Gloria Tesha, Inocent Charles, Fatuma Haji, Fikiri Keya, John James, Anna Kessy, Simon Andrew, Anna Edward, John Thadei, Regina Fredirik, Joram Kisera, Novelt John, Rose Pius, John  James, Anna Kessy, Joan Temba, Neema Kihisu, Regina Fredirik, na Joram Kisela.
        Majeruhi wengine ni pamoja na Neema Daud, Beata Cornel na Debora Joachim, Lioba Osward, Ropse Pius, Philimon Gereza, Kisesa Mbaga. Majeruhi wengi wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mount Meru na Hospitali Teule ya St. Elizabeth.
        Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo kuwa watulivu kipindi hiki na kuviachia vyombo vya usalama kuchunguza ili kuwabaini wahusika ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa pale inapobidi kufanikisha uchunguzi.
        Aidha ameomba msaada wa madaktari wa ziada kwa haraka kuwahudumia majeruhi kwani wengine wamejeruhiwa vibaya. “Tunatakiwa kuachia vyombo vya usalama pekee tuwe watulivu na tutoe taarifa kwa Polisi lakini pia tunaomba msaada wa madaktari wa ziada katika hospitali kwani hawa majerui wameumia vibaya sana,” alisema Magesa.
        Hadi sasa mtu mmoja amefariki dunia na zaidi ya majeruhi 50 wamegundulika kudhurika katika mlipuko huo. Majira ya saa nne asubuhi leo katika sherehe za uzinduzi wa Kanisa Kanisa jipya Katoliki la St. Joseph Mfanyakazi, hafla iliyokuwa ikiongozwa na Balozi wa Vatican nchini, Fransisco Padika na askofu Lebulu kumetokea mlipuko wa kitu kinachodhaniwa kuwa bomu kilichorushwa na mtu asiyejulikana

        Tuesday, April 16, 2013

        CAG Ataka William Mhando wa Tanesco na Mkewe Washitakiwe

         



        Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh (kushoto) akiwa na Rais Kikwete.
        MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh amemuweka kitanzini aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando, baada ya kushauri ashtakiwe pamoja na mkewe, Clara, kutokana ukiukwaji wa sheria katika kutoa zabuni.
        Mbali na Mhando, wengine ambao CAG amependekeza wachukuliwe hatua za kisheria ni Mkurugenzi wa Kampuni ya McDonald Live Line Technology, watu wote walioingia katika biashara na Tanesco kinyume cha sheria pamoja na wafanyakazi waliohusika kutoa zabuni hizo.
        Mapendekezo hayo ya CAG, Utouh yamo katika ripoti yake ya Ukaguzi wa Mashirika ya Umma ya 2011/12, aliyoiwasilisha bungeni wiki iliyopita ikirejea ukaguzi maalumu uliofanyika katika shirika hilo kutokana na maombi ya bodi ya wakurugenzi ya shirika hilo. CAG pia ameweka wazi kuwa Tanesco iligubikwa na ukiukwaji uliokithiri wa Sheria ya Ununuzi ya 2004 na kanuni zake za mwaka 2005, uliosababishwa na viongozi wake wa juu.
        “Mkurugenzi Mkuu wa Shirika akiwa ndiye mwenye uamuzi wa kuhusu ununuzi, alishindwa kuzuia ukiukwaji huu wa sheria ya ununuzi na mara nyingi aliidhinisha ununuzi wa chanzo kimoja au usiozidi ushindani,” inasema ripoti hiyo na kuongeza:
        “Bodi inatakiwa kuripoti kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DPP) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) yale yote yaliyogunduliwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kubaini kuwapo kwa rushwa na ubadhirifu.”
        Katika ripoti hiyo, CAG amebainisha ukiukwaji mkubwa wa sheria uliofanywa na Mhando, huku akibainisha kuwa mkewe, ambaye ni Mtendaji wa Mkuu wa Kampuni za Santa Clara Supplies Company Limited, alipewa zabuni katika shirika hilo kwa kutumia taarifa za kughushi. Pia CAG amebainisha kuwa kampuni hiyo haikuwasilisha katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), rejesho la kodi kiasi cha Sh4.854 milioni ilizolipwa na Tanesco.
        Santa Clara
        CAG amebainisha kuwa kampuni hiyo iliyosajiliwa Aprili 18, 2011, ilipewa Leseni ya Biashara, Mei 2011 na kwamba wakurugenzi na wanahisa wa kampuni ni mke na watoto wawili wa Mhando. Mke wa Mhando aliwahi kuwa mfanyakazi wa Tanesco, lakini aliacha kazi baada ya mumewe kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu.
        CAG amebainisha kampuni hiyo iliingia mkataba na Tanesco na kupewa zabuni Namba PA/001/11/HQ/G/011 ya ugavi wa vifaa vya ofisi, vifaa vya matumizi ya kompyuta na mashine za kudurusu, kwa mwaka 2011 hadi 2012, mkataba ulianza Desemba 20, 2011.