MKULO ASEMA HAWAJIBIKI KAMATI KUU CCM, NUNDU ATOA MANENO MAKALI, MAIGE, "NIACHENI"
Ramadhan Semtawa na Boniface Meena
SIKU chache baada ya Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kubariki uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete wa kulisuka upya Baraza la Mawaziri kwa kuwaondoa waliotajwa katika Ripoti Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), mawaziri wanaotakiwa kujiuzulu wamekataa kuchukua hatua hiyo huku mmoja wao, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo akisema hawajibiki kwa chombo hicho cha chama.
Kwa wiki mbili sasa, kumekuwa na shinikizo la kutaka mawaziri wanane wajiuzulu nyadhifa zao kutokana na wizara zao kutajwa na CAG kwamba zimehusika na ufisadi huku wengine wakitajwa moja kwa moja kufanya uamuzi wenye maslahi binafsi.
Wakizungumza na waandishi wetu kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya mawaziri hao walisema wanaacha hatima yao mikononi mwa Rais ambaye ndiye mamlaka ya uteuzi na kutengua nafasi zao.
Mkulo
Mwandishi: Asalaam alaykum ndugu yangu Waziri Mkulo.
Mkulo: Walaykum Salaam.
Mwandishi: Habari ya mapumziko?
Mkulo: Aaah salama.
Mwandishi: Nimekupigia kutaka kujua msimamo wako kuhusu uamuzi wa CC.
Mkulo: Nakusikiliza endelea.
Mwandishi: CC imebariki Rais Kikwete afumue Baraza la Mawaziri ni kwa nini usijiuzulu kabla?
Mkulo: No comment, (sina la kusema).
Mwandishi: Lakini, CC ina nafasi kubwa katika utendaji wa Serikali, kwa nini huoni uzito wa agizo lake?
Mkulo: Mimi sijaona muhtasari wa vikao vya CC lakini, pia siwajibiki kwa CC.
Mwandishi: Kwa maana nyingine huwezi kujiuzulu?
Mkulo: No comment katika hilo.
Mkulo amekuwa akitajwa kutaka kuvunja Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma (CHC) kwa madai ya kuficha kile kilichoitwa baadhi ya tuhuma za ufisadi katika uuzaji mali za umma ikiwemo Kiwanja Namba 10 kilichopo Barabara ya Nyerere, kwa Kampuni ya Mohamed Enterpises (MeTL).
Mkuchika
Mwandishi: Salaam ndugu yangu Waziri Mkuchika.
Mkuchika: Nzuri ndugu yangu
Mwandishi: Mimi ni...(jina la mwandishi) kutoka gazeti la ...(jina la Gazeti).
Mkuchika: Sawa nakusikiliza.
Mwandishi: Ndugu waziri, natambua rekodi yako nzuri ya utendaji wako serikalini, lakini nina swali.
Mkuchika: Sawa, uliza tu.
Mwandishi: Umewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, hivyo unajua nafasi chama serikalini.
Mkuchika: Ndiyo.
Mwandishi: Sasa, CC imebariki kuvunjwa Baraza la Mawaziri, je, huoni ni vyema ukakaa pembeni kabla?
Mkuchika: No comment.
Mwandishi: Lakini, unafahamu CC ni chombo kizito uliwahi kuwa mjumbe, kwa nini usubiri kufukuzwa na Rais?
Mkuchuka: Wewe bwana vipi? Uliniuliza nizungumzie uamuzi wa CC sasa nakwambia No comment huelewi?
Mwandishi: Nashukuru sana ndugu waziri
Mkuchika: Ahsante na wewe pia.
Waziri Mkuchuka anatakiwa kujiuzulu kutokana na tuhuma za ubadhirifu katika wizara yake kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo, ambazo ni pamoja na mtandao mpana wa wizi katika wizara hiyo huku Halmashauri ya Wilaya Kishapu pekee ikiwa imepoteza Sh6 bilioni.
Nundu
Mwandishi: Asalaam Alaykum Waziri Nundu.
Nundu: Walaykum Salaam.
Mwandishi: Pole na misukosuko ambayo ni kawaida katika siasa.
Nundu: Nashukuru sana ndugu yangu.
Mwandishi: Mimi fulani (jina) Nimekupigia, moja kukwambia tuko pamoja kwani sote ni ndugu, lakini nitakuwa na la pili.
Nundu: Nashukuru sana.
Mwandishi: Kwa hiyo, la kwanza, ndiyo hilo nakupa nguvu na ukubaliane na hali halisi.
Nundu: Sawa.
Mwandishi: La pili, juzi CC ya CCM ilibariki Rais avunje Baraza, je, huoni ni vyema ukajiuzulu kabla?
Nundu: Sikiliza wewe usijidai mjanja , hili ndilo la kwanza ulilotaka kuniuliza ukajidai unaanza kunipa pole.
Mwandishi: Hapana. Lakini huoni kujiuzulu unajijengea heshima kuliko kufukuzwa na Rais?
Nundu: Sikiliza kwanza, wacha kupapatika maana hunipi nafasi.
Mwandishi: Sawa endelea, lakini swali langu la msingi ni kuhusu agizo la CC ya chama unachotoka.
Nundu: Hayo ya CC sitaki kuyazungumzia. Lakini pia sitaki kuongea na ninyi Mwananchi mnapotosha ukweli.
Mwandishi: Sawa, kama tulipotosha ndo nakupa nafasi ueleze kwa usahihi.
Nundu: Ninyi sijui mnatumiwa na ..... kuandika uongo halafu mnajidai kutetea maslahi ya taifa.
Mwandishi: Ndugu Waziri, huoni kwa nafasi yako hutakiwi kusema maneno kama hayo?
Nundu: Ndiyo nimekwambia hivyo uandike sasa. Mnatumiwa na ... kunichafua.
Waziri Nundu anatuhumiwa kuipigia kifua Kampuni ya Chinese Merchants kwa ajili ya ujenzi wa gati Na13 na 14 katika Bandari ya Dar es Salaam huku akienda mbali na kumtuhumu Naibu wake, Athuman Mfutakamba kwamba amekuwa akishinikiza Kampuni ya China Communication Construction Company (CCCC), ipewe kazi ya kujenga magati hayo.
Maige
Swali: Mheshimiwa unaonaje uamuzi wa Kamati Kuu na msimamo wa Rais kuwawajibisha mawaziri waliotuhumiwa, kwa nini usiwajibike?
Maige: Siwezi kuzungumzia mambo hayo kwa sasa, nashukuru.
Wizara yake imekumbwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo uuzaji wa mazao ya misitu, ujangili na kusafirishwa wanyamapori nje ya nchi.
Nyalandu
Mwandishi: Habari yako ndugu Nyalandu?
Nyalandu: Safi kaka. Nani wewe?
Mwandishi: Mimi fulani (jina)...kutoka... (jina la gazeti).
Nyalandu: Sawa kaka nakusilikiliza.
Mwandishi: CC ya CCM imeamua Rais Kikwete avunje Baraza, je, huoni umuhimu kujizulu kabla hujaondolewa?
Nyalandu: Kwanza, nimpongeze CAG na vyombo vya habari, lakini, nasema hebu tuache mamlaka ziamue.
Mwandishi: Sawa, lakini uwajibikaji kisiasa ni jambo la heshima. Hili unalionaje?
Nyalandu: Mimi nadhani, kwa jambo hili lilipofikia, ni vyema waliotajwa moja kwa moja wawajibike. Ni jambo jema.
Waziri Nyalandu ameingia katika malumbano na Waziri wake, Dk Cyril Chami wakitupiana mpira kuhusu kashfa ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS), inayomkabili Mkurugenzi wake Mkuu, Charles Ekelege baada ya kudaiwa kuiingizia Serikali hasara ya karibu Sh30bilioni kutokana na ukaguzi hewa wa magari nje ya nchi.
Shikizo la mawaziri hao lilianzia bungeni baada ya wabunge wengi kutaka wawajibishwe kwa kuondolewa katika nyadhifa zao.
Katika kuongezea nguvu shinikizo lao, wabunge hao waliamua kuanzisha mchakato wa kumpiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Mchakato huo ambao ulikuwa ukisimamiwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe hadi Bunge linaahirishwa, wabunge 76 wakiwamo wa CCM walikuwa wameshasaini katika orodha hiyo.
Uamuzi huo wa wabunge pia uliridhiwa na kikao cha faragha cha wabunge wa CCM kilichofanyika Dodoma wakati Bunge likiendelea
Monday, April 30, 2012
Mawaziri wagomea uamuzi wa kamati kuu CC ya CCM, wasema hawawajibiki kwa chama
Mbunge wa Sumbawanga Mjini (CCM), Aeshi Hillary avuliwa Ubunge na Mahakama
|
Mussa Mwangoka, Sumbawanga MAHAKAMA Kuu Kanda ya Sumbawanga imetengua Ubunge wa Aeshi Hilaly (Sumbawanga Mjini- CCM) kuanzia jana.Hukumu hiyo ya kurasa 68, iliyosomwa na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Betwell Mmila na kuchukua saa tatu, imekuja siku chache baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kumvua Ubunge Godbless Lema (Arusha Mjini- Chadema). Akisoma hukumu hiyo, Jaji Mmilla alisema kati ya hoja 21 zilizowekewa pingamizi na aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Chadema, Nobert Yamsebo ni vipengele viwili pekee ambavyo mahakama hiyo imeridhia kuwa vina dosari katika uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 31, 2010. Alivitaja vipengele ambavyo vilikuwa na dosari kuwa ni pamoja na kuwepo kwa mazingira ya rushwa katika uchaguzi na kutokuwapo kwa mazingira huru katika kampeni kwenye baadhi ya maeneo ya jimbo hilo. Jaji Mmila alisema aliyekuwa mgombea wa CCM (Hilaly), alikwenda kwenye kikao cha ndani kilichodaiwa kuitishwa na viongozi wa CCM katika eneo Shule ya Msingi Kantalamba Mazoezi na kuwashawishi baadhi ya wapiga kura kwa kuwapa rushwa ya Sh15,000 na watu wapatao sita walikuwapo kwenye mkutano huo kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi. Eneo jingine ambalo lilitajwa kuwa na dosari ni kutokuwapo kwa mazingira huru katika mchakato wa kampeni kwenye Vijiji vya Mtimbwa na Kisumba ambako mgombea wa Chadema alizuiwa na baadhi ya wakazi wa eneo hilo kufanya kampeni zake baada ya kumfanyia fujo. Aidha, hukumu ya Mahakama hiyo imemtaka Hilaly kulipa gharama zote za kesi hiyo. Pamoja na hukumu hiyo, Mahakama hiyo imetoa fursa kwa upande wa mlalamikiwa kukata rufaa iwapo atakuwa hajaridhika na hukumu iliyotolewa. Katika hoja ya msingi, mlalamikaji aliiomba Mahakama kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo kwa madai kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu mbalimbali za uchaguzi. Walalamikiwa wengine katika kesi hiyo walikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Msimamizi Msaidizi na Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi. Katika kesi hiyo, mlalamikaji Yamsebo aliwakilishwa na kampuni ya kisheria ya Mkumbe Advocate and Company Ltd ya Mbeya huku upande wa Serikali ukiwakilishwa na wanasheria wawili wa Serikali, wakiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Paul Shahidi. Mlalamikiwa aliwakilishwa na jopo la Mawakili watatu, Juma Nassoro kutoka Kampuni ya Nassoro Advocate, Abubakar Salim wa Kampuni ya BLC Advocate na Ileth Mawalla kutoka S. Mawalla Law Consultant and Attorney ya Sumbawanga. Baada ya hukumu Huku hiyo ilivuta hisia za wakazi wengi wa Mji wa Sumbawanga na vitongoji vyake na baada ya kutolewa, vijana wa Chadema walianza kushangilia baada ya kufahamu kwamba Mahakama imetengua ubunge huo. Hata hivyo, Wakili Nassoro alisema mteja wake anakusudia kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo baada ya kutathmini mwenendo mzima wa kesi hiyo. Kwa upande wake, Yamsebo alisema kilio cha wanyonge kimesikika na Mahakama imetenda haki hali ambayo inawafanya wananchi kuendelea kuwa na imani na mhimili huo wa dola. Katika matokeo ya uchaguzi huo yaliyotenguliwa, Hilaly alishinda kwa kura 17,328 dhidi ya Yamsebo aliyepata kura 17,132. Nje ya ukumbi wa Mahakama, wafausi wa Chadema walipiga kelele za furaha na kushangilia hali iliyomlazimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Isuto Mantage kuchukua kipaza sauti na kuwataka kutulia. Mashabiki hao wa Chadema walitii amri hiyo lakini kwa kutoka nje ya geti la kuingilia mahakamani na kuendelea kushangilia. Waliendelea kushangilia kwa kupita katika mitaa kadhaa ya mjini hapa. Uchaguzi huo ulikuwa wa kwanza kwa Hilaly kuingia bungeni mwaka 2010. Kijana huyo alipata elimu yake ya msingi katika Shule ya Jangwani Sumbawanga kuanzia mwaka 1983 hadi 1989. Chadema chatoa tamko Baada ya kupata taarifa za hukumu hiyo, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika aliitisha mkutano wa waandishi wa habari Ofisi za chama hicho, Kinondoni, Dar es Salaam na kusema sasa kinasubiri Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kutangaza tarehe ya uchaguzi. “Tunachosubiri ni tume tu itangaze tarehe ya uchaguzi ili mgombea wetu ambaye hakutangazwa tu katika uchaguzi ule akatangazwe mshindi” alisema Mnyika na kuongeza: “Katika uchaguzi ule mgombea wetu hakutangazwa tu, lakini kati ya majimbo tuliyoyataraji ni pamoja na Sumbawanga Mjini. Ndiyo maana mgombea wetu alifungua kesi nasi tukaunga mkono hatua hiyo kwa sababu tulijua haki haikutendeka. |
Tundu Lissu aanza mashambulizi upya
Mbunge Tundu Lissu akihutubia mkutano viwanja vya stendi ya zamani mjini Singida, tangu mahakama kuu impe ushindi dhidi ya kesi
Wafuasi na wapenzi wa CHADEMA wakiitikia kukunja ngumi juu kuonyesh nguvu ya umma katika mkutano huo, mbele ni mtoto Hilda Jack
Mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu(wa pili kulia),akiingia kwenye viwanja wa stendi ya zamani mjini Singida kwa ajili ya mkutano
Mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu akimtolea mfano muuza maji mjini Singida kwa kutumia toroli, maarufu kwa jina la 'Chai
Aprili 30,2012.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa wito kwa viongozi na wanachama ‘safi’, walio ndani ya CCM, wajiunge mapema na CHADEMA ili waikomboe nchi, kutoka kwa wezi na mafisadi wa fedha za umma.
Mnadhimu mkuu, kambi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu, alitoa rai hiyo kwenye mkutano wa hadhara, aliufanya eneo la stendi ya zamani, mjini Singida, kwa lengo la kukiimarisha chama, bada ya kushinda kesi yake ya uchaguzi.
Lissu ambaye pia ni mbunge Singida mashariki, aliwashauri wajiondoe mapema, badala ya kung’ang’ania huko, kusubiri CHADEMA itawale nchi, halafu ndio wajitokeze kusema na wao ni wafuasi wa chama hicho.
Pia aliwaomba viongozi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA hivi sasa wachukue tahadhari, vinginevyo watapata madhara makubwa, ikiwemo hata kupoteza maisha yao.
Alisema kitendo cha kuuawa kwa mwenyekiti wao huko Usa river, mkoani Arusha na kukatwa katwa kwa panga wabunge wa CHADEMA mkoani Mwanza, ni onyo kwa wanachama na viongozi wa chama hicho.
“Vita hii ni kubwa, lazima tuielewe, kuanzia sasa kaeni chonjo, vinginevyo CHADEMA tutauawa, mwenyekiti wetu kule Arusha amechinjwa na wabunge wetu huko Mwanza wamekatwa katwa mapanga, tena mbele ya polisi….tuangalie sana,”alitahadharisha Lissu.
Kuhusu ushindi wa kesi iliyomkabili, ambayo ni moja ya mashauri 14 yaliyofunguliwa, kati ya majimbo 23 ya CHADEMA nchini, Lissu aliishukuru mahakama kumuona hana hatia, ingawa anaamini wadai wamepoteza fedha nyingi, zinazofikia zaidi ya Sh. Milioni 200, ili ubunge wake utenguliwe.
Huo ulikuwa mkutano wa kwanza kufanyika Singida mjini na watatu kimkoa, tangu mahakama kuu, kanda ya Dodoma, kupitia Jaji Moses Mzuna wa Moshi, Mkoani Kilimanjaro, kufutilia mbali shauri la kupinga ubunge, alilofunguliwa na wanachama wawili wa CCM.
Kwa hisani ya Mjengwa!
CHEKA ASHINDA GARI BAAADA YA KUMTWANGA MAUGO
Jana usiku katika ukumbi
wa PTA, Dar es Salaam kulifanyika mpambano wa kuwania ubingwa wa IBF
kati ya Francis Cheka (Morogoro) na Mada Maugo (Dar es Salaam).
Pambano hilo lilikuwa la raundi 12 lakini ilipofika raundi ya sita kabla ya kuanza raundi ya saba, Maugo alitangaza kutokuendelea na mchezo kwa kile alichodai kuishiwa na pumzi na kusema, '...sirudi, jmaa ataniua...' huku akivua "gloves" na hivyo kumpa Cheka kwa Technical Knock Out "TKO", uamuzi ambao ulimpa Cheka mkanda wa Ubingwa wa IBF pamoja na gari (pichani).
Furaha ya ushindi huo imegeuka huzuni leo baada ya Cheka kupata ajali ya gari hilo alilokabidhiwa jana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, akizungumza na "SufianiMafoto" alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea jana usiku majira ya saa nane maeneo ya Manzese na kuwajeruhi dereva na abiria wake waliokuwa katika pikipiki hiyo. Alisema baada ya ajali, dereva wa gari hilo lenye namba za usajili T 321 AAU, aliyefahamika kwa jina la Francis Cheka, alifikishwa kituo cha Polisi cha Oysterbay na kushikiliwa hadi asubuhi ya leo walipofika ndugu zake na kumwekea dhamana.
Akielezea tukio hilo la ajali, Kenyela alisema kuwa gari la Cheka lilikuwa likitokea maeneo ya Manzese kuelekea Ubungo na pikipiki ilikuwa ikitokea Ubungo kuelekea Manzese na walipofika maeneo ya Tip Top Manzese, dereva wa pikipiki alihamia barabara ya pili ili kuelekea Ubungo na ndipo alipogongana na gari hilo. Aidha alisema kuwa dereva huyo wa pikipiki bado amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala akiendelea na matibabu huku abiria wake akitibiwa usiku wa jana na kuruhusiwa.

Source: http://www.wavuti.com
TAMKO LA WANACHAMA WA CHADEMA MAREKANI
TAMKO LA WANACHAMA WA CHADEMA MAREKANI
KUHUSU MATUKIO YA KUUAWA KWA WANACHAMA NA WAPENZI WA CHADEMA
Kumekuwa na mfululizo wa matukio ya kinyama ya kuuawa kwa Wanachama, Viongozi na wapenzi wa CHADEMA hasa katika vipindi vya chaguzi. Matukio yote haya hutokea kwenye vipindi vua chaguzi ndogo au baada ya chaguzi hizo. Kuna taarifa kwamba katika baadhi ya Matukio jeshi la Polisi hutaarifiwa lakini hawachukui hatua zozote stahiki kulinda Usalama wa Raia hosusani wanachama wa CHADEMA kama Raia wengine. Kutokana na mfululizo wa matukio haya ni dhahiri kabisa kuna mpango wa kutaka kuwatisha Raia wapenda haki wasifanye maamuzi ya Kidemokrasia kwa kushirki katika chaguzi hizo kwa kujazwa hofu kutokana na Matukio haya yanayojili.
Kila mara kunapotokea matukio haya Jeshi la Polisi huishia kusema kuwa wanafanya Uchunguzi kujua nani wanahusika na kufanya Matukio haya ya kinyama pasipo kutoa taarifa zozote kwa wananchi wala kuonyesha jitihada zozote za kuwakamata wahusika; Matokeo yake uchunguzi wa matukio hayo ukiwa hauna mafanikio yeyote ya kuwakamata na kuwafungulia mashtaka wahusika.
Kutokana na hali hiyo wananchi wengi wamekuwa hawana Imani na jeshi la polisi kwani hakuna hata tukio moja kati ya matukio ya mauaji ya kinyama yaliyokuwa na mafanikio ya kuwakamata wahusika.
Kuna sababu nyingi za kuhusisha matukio haya na masuala ya kisiasa kwa sababu ya Mazingira ya matukio haya jinsi yanavyotokea. Kwanza yanalenga kwa wanachama, Viongozi na wapenzi wa CHADEMA tu. Naweza kutoa ushahidi kwa tukio lililotokea kwenye Uchaguzi Mdogo wa Igunga kwa kuuwawa kinyama kwa msimamizi wa kura wa CHADEMA aliyetekwa nyara na watu wasiojulikana hatimaye kukutwa porini akiwa ameuawa kinyama kwa kupigwa na vitu kama mawe na kumwagiwa tindikali.
Ushahidi wa pili ni wa lile tukio la kupigwa Mapanga kwa Wabunge wawili wa CHADEMA Mheshimiwa Silvestre Machemli na Mheshimiwa Hayness Kiwia kwenye Uchaguzi mdogo wa diwani wa Kirumba Mwanza. Siku ya tukio waheshimiwa hawa walipogundua kuwa wanafuatiliwa na watu waliowatilia mashaka walipiga simu Polisi kuomba msaada lakini kilichotokea Polisi walichelewa kufika sehemu ya tukio na hata walipofika waliwashuhudia waheshimiwa hawa wakiwa wamezungukwa na watu wasiojulikana na kupigwa mapanga bila hata Polisi kuchukua hatua zozote. Je, hili linaashiria nini? Kitendo cha Polisi kushuhudia Raia mwema tena Mbunge akiwa anapigwa mapanga mbele ya macho yao wasichukue hatua zozote?
Ushahidi wa tatu ni wa lile tukio lililotokea Arumeru la kupatikana miili ya watu wanne wanaosemekana kuuawa kwa kunyongwa na kutupwa karibu na shule moja ya Msingi huko Arumeru. Bila kusahau tukio la Mwanachama mmoja wa chadema aliyekamatwa na kutekwana watu wasiofahamika na kuteswa na kuachwa na majeruhi makubwa na kutupwa kando ya mto hatimaye kuokotwa na mpita njia.
Mfululizo wa matukio haya na mengne ya kupotea kwa kutekwa Wanachama na wapenzi wa CHADEMA ni ishara tosha kwamba kuna mpango ulioandaliwa wa kufanya uhalifu huu kwa Wanachama wa CHADEMA na Jeshi la Polisi linafahamu hilo.
Je, Watanzania Siasa ndio inatupeleka huko? Tuna vyombo mbalimbali vya ulinzi ikiwemo Idara ya Kijasusi (Usalama wa Taifa). Je, wanatoa mchango gani kuhusiana na matukio haya yanayoendelea?
Vyombo vya Usalama likiwemo jeshi la Polisi kumbukeni matukio haya yanawapata Watanzania wasio na hatia ambao ni Kaka zenu, wajomba zenu, dada zenu na Shangazi zenu. Kuyafumbia macho matukio haya itapelekea siku moja Wananchi watachukua Sheria mkononi na kusababisha machafuko makubwa ambayo yatasababisha umwagaji mkubwa wa damu wa kulipiza kisasi.
Watanzania hatuna utamaduni huo wala hatupendi yaliyotokea kwa jirani zetu wa Rwanda na Burundi yatokee hapa. Huko yalikuwa na masuala ya ukabila hapa yanaweza kuwa masuala ya itikadi za Kisiasa.
Masuala ya kisiasa yamesababisha machafuko makubwa katika nchi za Kiarabu kama Tunisia, Misri, Yemen na sasa Syria. Kwa kweli hatupendi hayo yatokee kwetu.
Kufumbia macho matukio hayo ni kujenga chuki kwa Wananchi dhidi ya Jeshi la Polisi. Pia wananchi kuchukiana wenyewe kwa wenyewe kwa sababu za itikadi za kisiasa. Vyombo vya Ulinzi hususani Jeshi la Polisi na Idara ya Usalama lazima wachukue hatua stahiki kukabiliana na matukio haya ya kinyama, vinginevyo tutarajie umwagaji mkubwa wa damu wa kulipiza kisasi.
WANACHAMA WA CHADEMA MAREKANI
Source: http://www.wavuti.com
NYUMBA HII INAPANGISHWA KWA SH,10,000 KWA MWEZI
HAPA WANAFUNZI HUJISOMEA KWELI USIKU?
Majibu ya Kigwangalla: Kwa Nini Sikusaini Hoja ya Mhe. Zitto Zuberi Kabwe (MB)
Ndugu zangu wanabodi,
Nimeamua kuja kujibu kama ambavyo mngependa nifanye. Siyo kwamba nimekimbia JF, la hasha. Siwezi kukimbia na wala sina sababu ya kufanya hivyo. Ni kwamba gadget yangu ninayotumia kwa mawasiliano ilipata mushkeri na nikawa nalazimika kutumia kompyuta na bahati mbaya sana kwa jinsi nilivyokuwa bize na ujenzi wa Taifa nilijikuta nakosa muda wa kukaa kuanza ku-surf. Nisamehewe kwa hilo.
Mimi sijawahi kuwa mnafiki, at least kwa alama tatu za mnafiki kama tunavyofundishwa sisi waislamu. Kwa faida ya mjadala huu, niseme alama zenyewe. Moja ni kuwa akitoa ahadi hatekelezi. Mbili, ni akiaminiwa anahalifu na tatu, akizungumza husema uongo. Namshukuru Mungu sina hata moja ya alama hizi na hivyo kushindwa mtihani wa kuwa 'mnafiki'. Ungeniita mnafiki kama nisingekuwa tayari kutoa maelezo ya maamuzi yangu, ama kama ningewasaliti CCM na kupeleka siri za huku kule, ama kama ningeahidi kuunga mkono hoja hiyo kisha nikakimbia. Leo hii mimi niko chama kimoja tu, CCM, na nitafanya mambo yanayokubalika ndani ya CCM. Siku nikihamia CHADEMA/CUF/NCCR basi nitafanya ya huko bila kusaliti kule na kurudisha CCM ama kupeleka kokote kule kinyume na utaratibu. Huo ndiyo msimamo wa ukweli na siyo unafiki.
Kuna uwezekano wa kuwa na tafsiri tofauti kutokana na pre-conceptions zetu vichwani, siwezi kulizuia hilo hata kidogo. Kwa kuwa ninakalia kiti cha uwakilishi, nina-feel ninawajibika kwenu kutoa maelezo ya msimamo wangu kwenye hili, na wala sintomumunya maneno.
Kwanza, hoja yenyewe siikubali. Kwa sababu ninaamini serikali ya Chama Changu (CCM) haijashindwa kufanya kazi ya watanzania kiasi cha kung'olewa madarakani kwa namna hiyo. Pili, naamini na ninakubali, na kwa hakika ninakerwa na baadhi ya watu waliopewa dhamana za kuongoza baadhi ya ofisi nyeti za umma wametuangusha watanzania, na hivyo naunga mkono hoja ya kutaka kuwatoa hawa. Mhe. Zitto Kabwe (MB) alipokuwa akijumuisha hoja yake, alitaka serikali iwawajibishe baadhi ya mawaziri na watendaji wakuu wa Wizara na Mashirika ya umma, na akasema kama serikali haikufanya hivyo kufikia J3 iliyofuata basi sisi (Bunge) tuna uwezo na WM na kwamba atapitisha karatasi ya kukusanyia saini 70 ili kukidhi matakwa ya kikanuni ya kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na WM; kwa tafsiri yangu ni kwamba Mhe. Mbunge alilenga kuweka presha kwa serikali, kuitaka iwajibike kwa kuwawajibisha mawaziri hao (watano) kama alivyowataja yeye. Kwanza mwanzoni nilielewa hivyo. Baadaye jinsi ilivyopokelewa na wadau mbalimbali nikaona kama hoja inahama sasa na kwamba si mawaziri hao watano wenye tuhuma mbalimbali, ni PM na kwa maana hiyo ni serikali yote Bungeni! Hili mimi siliungi mkono na silikubali. Nasema wazi hivyo kwa sababu, mimi nina imani na WM, nina imani na Rais - aliyemchagua WM, na nina imani na Mawaziri wengine wengi wazuri tu kwenye serikali hii, na msimamo wangu huu uko wazi sana tu.
Mbili, sioni sababu ya kuiingiza nchi kwenye wasiwasi wa kiutawala kiasi hiki. Na kwa kuwa wabunge wa CCM kwenye party caucus tulikuwa tayari tumeishaambiwa kwamba kuna mawaziri wameamua kujiuzulu wenyewe (tena siyo wale watano, ni wanane kabisa) kutokana na tuhuma hizo na presha kutoka kwa wabunge wa CCM na wengine, sikuona sababu ya mimi kusaini hoja ya Zitto (ambayo kikanuni ilikuwa imekosewa - kitendo kilichonidhihirishia wazi kwamba hakuwa na u-seriousness wa kutaka kweli kumuondoa WM bali ni baadhi ya mawaziri, sema alichomeka tu hiyo kauli ili kutia presha zaidi!). Zaidi ya hapo, ninaamini hoja hiyo ni nzito na kimsingi, kwa sasa, imegeuka kuwa ni mchezo wa kisiasa na media na haitofika popote! Kama Mhe. Mbunge Zitto alikuwa na nia ya dhati ya kumuondoa WM asingekurupuka kiasi kile, angewashirikisha watu wengi zaidi, hususani wabunge wa CCM, na kimkakati zaidi angewapa wabunge wa CCM walioibua hoja hizo za kuwataka mawaziri wang'olewe na hapo angefanikisha malengo ya kumuondoa WM na serikali yake Bungeni. Kwa namna ilivyo hawezi kupata support ya wabunge wa CCM na kwa kuwa sisi ndiyo majority, hoja hiyo haitopita - na hii itaturudisha kule kule kwenye nilichokisema kule twitter kwamba hoja hii ni ......politically right but technically flawed!
Jamani, hoja ya kumuondoa WM madarakani siyo kitu kidogo, siyo kitu cha mchezo, ni lazima ujipange. Ukweli ni kwamba rafiki yangu Mhe. Zitto hakujipanga kuifanikisha (bila shaka yeye mwenyewe analielewa hili vizuri - he is smarter than this, I know him!)
Tatu, msisahau kitu kimoja cha muhimu kabisa. Kwamba, mimi ni Mbunge kutokea CCM na kama walivyo wengi wenzangu hatukusaini kwa sababu hatuwezi kuiangusha serikali ya CCM kwa hoja inayoletwa na Mbunge wa Kambi ya Upinzani! Mbunge wa Chama Tawala kuamua kuiangusha serikali ya chama chako ni sawa na kuamua kukata tawi la mti uliokalia, kwa vyovyote vile utaanguka nalo! Simple logic! Mfumo wa Bunge letu ni wa Westminster, na hivyo kuna kambi ya Upinzani (yenye interest ya kutaka kuiangusha serikali inayotawala) na Kambi ya Serikali (ambayo ina interest ya kutaka kuilinda serikali yake). Kwa maana hiyo sisi wabunge wa CCM tuna jukumu la kuilinda Serikali inayopatikana kutokana na sisi kuwa majority. Serikali ni lazima i-enjoy majority status ndani ya Bunge ili nchi itawalike kwa amani na utulivu, japokuwa haimaanishi kuruhusu ubadhirifu na ndiyo maana kwenye Party Caucus wabunge wana nguvu na fursa ya kusema chochote dhidi ya serikali ya Chama Chao. Kuna wengine wanataka Bunge liwe Bunge huru (ama 'An Indipendent Power House') disregarding political opinions/inclinations/affiliations na serikali iwe serikali, hii haiwezekani kwa katiba tuliyonayo leo. Tubadilishieni kwanza katiba na mfumo wa kufanya kazi ndipo mtutake tufanye hayo mnayoyatamani.
Nadhani nimejiweka wazi bila unafiki, sasa tujadili kwa hoja siyo kwa hisia na matusi kama hatukwenda shule vile.
Wakatabahu,
HK.
Friday, April 27, 2012
M/KITI WA KAMATI YA MAHUSIANO YA UVCCM MKOA ARUSHA AHAMIA CHADEMA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. TAARIFA KWA VYA HABARI
Ni muda mrefu nimeitafakari dhamira yangu na sasa ni wakati muafaka kufikia maamuzi magumu, Nimeamua kuachia nyadhifa zangu zote ndani ya CCM ambazo ni, MJUMBE WA MKUTANO MKUU CCM TAIFA, MJUMBE WA BARAZA LA MKOA UVCCM, NA M/KITI WA KAMATI YA MAHUSIANO YA UVCCM MKOA ARUSHA.
Yaliyonisukuma ni mwelekeo mbaya wa CCM kwa sasa ambao umejiondoa kuwa Chama cha wanyonge na wakulima na sasa ni chama cha kundi la watu wachache na watoto wao ndio sababu yanayoendelea sasa ndani ya CCM yanasikitisha sana.
Usaliti na makundi ndani ya CCM yanatishia kabisa uhai wa chama na tayari yamekwisha angamiza Taifa letu, hata hivyo nafasi ya wa watoto wa wanyonge ndani ya CCM inazidi kuwa finyu, aidha ujipendekeze kwa wakubwa ili upate nafasi ya kutumikia jamii au Chama, wakati nafsi yangu haiko tiyari kusimamia uovu huu sasa nimeamua kusimamia ninachokiamini bila uoga wala unafiki, na mfano Tazameni yanoyoendelea ndani ya UVCCM ARUSHA mikono ya mtoto wa mkubwa unaumaliza umoja huo mkoani hapa.
Lakini pia uzito wa serikali ya CCM kushidwa kuwawajibisha wabadhirifu na wanaotumia vibaya madaraka waliyopewa angalia ubadhirifu mkubwa hivi karibuni uliofanywa na Mawaziri na Watumishi wengine wa Umma, Angalia jinsi Serikali imelichukulia suala la Jairo kwa mzaha, ni hatari kwa Nchi yetu kwamba wakati watoto hawana madawati wako viongozi wakubwa ambao wanashindwa kuchukuliwa hatua kwa wizi wa mabilioni ya fedha.
Sababu ni nyingi sana za kwanini nimeamua kutoka CCM, nikisema niandike zote pengine itanipasa kuandika kitabu hata hivyo ninaamini kuwa nitakuwa na fursa ya kueleza mambo mengi sana kwenye mikutano ya hadhara nitakayofanya na Chama cha kipya CHADEMA.
CHADEMA ,nawashukuru kwa kunipokea na wahaidi utumishi na kazi iliyotukuka, nitajifunza kwenu na pia naamini mtajifunza kwangu ili tuweze kwa pamoja kuleta matumaini kwa wanyonge.
Kwa marafiki zangu na wanachama wa CCM, msihuzunike sana kwani ninatangulia kwenda kuwaandalia makao kwani ninajua nanyi pia mko njiani mnakuja ,hata hivyo sikuwahi kuwa mwema kama malaika tulipokuwa pamoja CCM naamini kuna mahali niliwakosea kama binadamu naomba msamaha kwenu na undugu wetu ubaki , lakini kama maamuzi yangu ya kwenda Chadema yatakuwa yamewauzunisha poleni sana na muendelee kuchukia kwani hatuwezi kuukwaza utu na faraja ya Mwanadamu kwa kufurahisha nafsi za watu wachache.
Asanteni sana karibuni Chadema.
Ally Bananga.
……………………
27/4/2012.
Neno La Leo: Bunge Ni Eneo La Umasikini!
Ndugu zangu,
Hapo
juu ni nyumba ya Waziri Maige na chini ni nyumba ya kabwela Mtanzania.
Na Spika wa Bunge, Anne Makinda alipata kutamka, kuwa Bunge ni eneo la
umasikini. Astaghafilulahi! Haki ya Mungu, ukistaajabia ya Mussa
utayaona ya Firauni.
Na jana, bila haya, Waziri Maige amekaririwa akiyasema haya;
"Akizungumza
na gazeti hili jana, Waziri Maige alisema hakununua nyumba hiyo kwa
Dola 700,000 kama inavyodaiwa, bali alinunua kwa Dola za Marekani
410,000.
Mbali
ya kukiri, alifafanua jinsi alivyoinunua na kuonyesha nyaraka
mbalimbali huku akieleza kuwa sehemu ya fedha alizonunulia, zilikuwa za
mkopo kutoka Benki ya CRDB.
Alisema mwaka 2005 alipoanza kuwa mbunge alipata mkopo na yeye na wenzake watatu, waliunda kampuni ya kusafirisha mzigo ya Splendid Logistic na kuanza kununua magari matatu na baadaye magari hayo yaliongezeka na kufikia saba.

Waziri wa Maliasili na Utalii,Ezekiel Maige
Alisema
Septemba, 2010 mwenzao mmoja alijitoa katika kampuni hiyo na hivyo
wakaamua kugawana mali kwa kuzingatia mtaji wa kampuni. Alipata magari
mawili na mwenzake manne na kuongeza kuwa gari moja kati ya hayo saba
lilipata ajali.
Alisema baada ya hapo aliamua kuanzisha kampuni nyingine ya kusafirisha mizigo ambayo inaendeshwa na mke wake... “Kampuni hiyo inaitwa Mem Logistic na ina magari mawili.”
Alisema magari hayo aliyakodisha kwa kampuni nyingine ya Bravo Logistic ambayo kila mwezi inamlipa Dola 20,000.
Alisema alipochaguliwa tena kuwa mbunge mwaka 2010 aliamua kutoongeza magari katika kampuni yake na kuanza kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba.
“Baada ya uchaguzi nilichukua mkopo wa Sh200 milioni katika Benki ya CRDB, baadaye Ofisi ya Bunge ilinikopesha Sh90 milioni kwa ajili ya kununua gari, fedha hizo zote nilizichukua na kuzihifadhi,” alisema Maige.
“Hizo fedha nilikaa nazo nikawa nataka kujenga nyumba baadaye nikaona nitafute nyumba ya kununua tu. Baadaye dada yangu, Angelina Ngarura ambaye ana kampuni ya kuuza matrekta, Dar es Salaam alinifuata na kuniomba fedha hizo kwa ajili ya kuzizungusha na tukakubaliana kuwa atakuwa akilipa riba ndogo kwa makubaliano kwamba siku yoyote nikizihitaji nitazichukua,” alisema.
Alisema ndipo alipopata nyumba iliyokuwa ikiuzwa Dola 450,000 lakini alikubaliana na muuzaji na kuuziwa kwa Dola 410,000.
Alisema katika ununuzi huo, hakuwa na kiasi hicho cha fedha kwani nyingine zilikuwa katika mzunguko katika kampuni ya dada yake na hivyo kuamua kwenda kukopa Dola 200,000 katika CRDB.
Alisema baada ya kupewa fedha hizo za mkopo, hati ya nyumba hiyo ilibaki benki kwa makubaliano kwamba akishindwa kulipa, benki itaichukua.
“Tuliingia mkataba na CRDB kulipia nyumba ile kwa miaka minne na mpaka sasa hivi nalipia Dola 5,127 kila mwezi, haya yote yapo kwa Kamishna wa Maadili,” alisema Maige.
Huku akionyesha mikataba ya ununuzi wa nyumba hiyo, nyaraka za mkopo wa benki, Maige alisema awali, alikuwa na magari mawili ambayo aliamua kuyauza na kununua gari nyingine aina ya BMW kwa Sh70 milioni.
Alidai kwamba kama kuna mali kinyume na hizo yuko tayari kuapa hata kwa Biblia Takatifu na kusisitiza kuwa hivi sasa kuna mapambano ya kisiasa ndiyo maana shutuma dhidi yake zinaibuka kila kukicha.
“Ukisikia mali zangu tofauti na hizo ni uongo ndugu yangu na kwa mkopo niliochukua wakati nikiwa mbunge sina hela mpaka Juni 2015,” alisema na kuongeza:
“Nikijiuzulu ubunge leo hii maana yake ni kwamba itakuwa kazi kweli na sitaweza kulipa mkopo. Sijakopa kwa kivuli cha ubunge wangu, nimekopa kama Maige kwa sababu kiwango cha kukopa bungeni nimeshakimaliza.” ( Mwananchi, Aprili 26, 2012)

Swali la Watanzania wengi ni hili; " Hivi Rais anasubiri nini kupangua Baraza lake la Mawaziri?"
Na hilo ni Neno La Leo:
Maggid Mjengwa
Lissu aitimulia vumbi CCM Babati, 1500 wajiunga Chadema
WanaCCM 1500 Wajivua magamba na kuvaa magwanda
Iringa nako Chadema yapangua gear kuongeza kasi
Akindole alisema sababu kubwa iliyomfanya kuhamia CHADEMA ni kuona uongozi wa CCM wa sasa ukiwanyanyasa wananchi kupita kiasi na kunyamazishwa pindi wanapokuwa na maneno ya kushauriana juu ya maendeleo ya kijiji chao. “Kwa sababu hiyo mimi nimeamua kutoka kwenye Chama cha CCM na kuhamia CHADEMA ili nijaribu kuona msimamo unakwendaje, maana tunanyanyaswa kupita kiasi na tukitaka kulalamika serikali haitusikilizi, na mbunge akija hapa tukilalamika hata yeye hatusikilizi. Mimi nilikuwa na mambo yangu mengi tu nimelalamika mpaka wilayani lakini sikusikilizwa. Tufanyeje wananchi?’’ alisema Japhet.
Kwa upande wake mzee Tula amesema kuwa, wakati wa uongozi wa Mwalimu Nyerere kulikuwa na viongozi waliokuwa wamepata mafunzo ya uongozi kwa lengo la kuwasaidia wananchi lakini kwa sasa wananchi wakilalamika viongozi hawatoi msaada wowote zaidi ya kukandamizwa kutokana na viongozi wengi kukosa maadili ya uongozi. “Hapa nilipo nina miaka 75, mzee kama mimi sikuwa na haja ya kuhama hama chama, lakini ninatafuta msaada, kama CCM kungekuwa na msaada viongozi wasio bora wangekuwa wanaonywa na kufuata maadili ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwa kweli nisingehama,“ alisema Tula.
Aidha, wazee hao wamesema kuwa, licha ya wao kuhamia CHADEMA, lakini bado wanaiomba serikali kumchukulia hatua mwenyekiti huyo wa Kijiji cha Kihesa Mgagao ambaye pia ni diwani wa kata na mwenyekiti wa CCM, kwani hawatendei haki wazee wa kijiji hicho na wananchi kwa ujumla na uongozi wake ni wa kidikteta.
CHADEMA yaiburuza CCM Uchaguzi Geita
Huko Chato, katika Mkoa mpya wa Geita, CHADEMA kimepata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa wenyeviti wa serikali za vijiji baada ya kuibwaga CCM kwa kupata vijiji vinane kati ya 11 vilivyokuwa vikishindaniwa. Uchaguzi huo mdogo wa kuziba nafasi zilizoachwa wazi na baadhi ya viongozi waliokuwepo awali jimboni humo kutokana na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vifo ambao ulifanyika hivi karibuni uliwafanya baadhi ya Wana CCM kujiunga na CHADEMA mara baada ya matokoeo kutangazwa akiwamo aliyekuwa mgombea wa CCM wa Kijiji cha Minkoto.
Nafasi zilizogombewa zilikuwa zikishikiliwa na viongozi wa CCM kabla ya baadhi yao kujiuzulu, kuhamia vyama pinzani na wengine kuhama makazi yao na kwenda maeneo mengine. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, msimamizi msaidizi wa uchaguzi huo, Sodio Nyuga alisema CHADEMA kimefanikiwa kutwaa nafasi 8 za vijiji dhidi ya tatu zilizonyakuliwa na CCM . Hata hivyo, CCM ilijifariji kwa kutwaa uenyekiti katika vitongoji 28 na CHADEMA kikipata nafasi 10, wakati wajumbe wa serikali za mitaa CCM kilijipatia wajumbe 92 na CHADEMA 46.
Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Chato, Mange Sai, alisema ushindi uliopatikana ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa wilaya hiyo kwa kuwa baadhi ya vitongoji CHADEMA ilipitisha wagombe pasipo kuwa na upinzani wa chama tawala jambo ambalo linaonyesha wazi kukubalika kwa chama hicho kwa wananchi. Alisema kuwa CHADEMA kilitegemea kuibuka kidedea katika uchaguzi huo mdogo kutokana na wapiga kura kuchoshwa na ahadi mbalimbali za serikali ya CCM ambazo zimekuwa hazina utekelezaji na badala yake baadhi ya viongozi wamekuwa wakijinufaisha kwa maslahi yao binafsi huku wakiwaacha wananchi wakitaabika.
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) kimezidi kupoteza nguvu zake sehemu mbalimbali
nchini, baada ya waliokuwa viongozi na makada wake ngazi za vijiji na
wilaya kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Habari
kutoka mikoa ya Manyara, Iringa na Kagera zimesema kuwa wimbi la
kukimbia kwa wanachama wa CCM na kujiunga na upinzani limeshika kasi
kuliko mwaka wowote tangu kuingia kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa.
Huko Babati zaidi ya wanachama 1,500 wa CCM wakiwamo wenyeviti wa vijiji wilayani Babati wamekihama chama hicho na kujiunga na CHADEMA, wakati wa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu. Kati ya waliojiunga na CHADEMA ni pamoja na Bi. Zamda ambaye ni kada maarufu wa CCM mjini hapa, Wakili Lumambo na wenyeviti wawili wa vijiji vya Mruki na Hala, ambao walijiunga na wanachama wao zaidi ya 100.
Akihutubia mkutano huo, Lissu amewataka wananchi wa Jimbo la Babati Mjini na wengineo kuiga mifano ya waliokataa kuonewa na kunyanyaswa na serikali ya CCM badala yake wachukue hatua ili kuondoa uvundo, wizi na uozo unaoendelea kufanywa na watawala.“Hatujaweka mkataba wa kuibiwa na serikali ya CCM kwa kipindi cha miaka mitano mitano, kwa hiyo hatuhitaji kusubiri hii miaka mitatu ya uchaguzi iliyobaki. Wakati umefika sasa wa kuchukua hatua, tukianzia na hili suala la mawaziri wanane, na pamoja na umaskini wetu tukiamua kusema kwa pamoja hakuna mtu atakayeweza kutuzuia,” alisema Lissu.

Huko
Iringa, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kihesa Mgagao, Kata ya Ngúruwe,
wilayani Kilolo, Isdori Kindole na wazee wawili, Tula Dumba (75) na
Japhet Ngoda (88) wamejiunga na CHADEMA kutokana na kile walichodai kuwa
wameshindwa kupata haki ya kweli kutoka katika chama hicho kupitia
uongozi wao wa kijiji hususan diwani wao kutuhumiwa kuhujumu mali za
umma. Wazee hao wamedai kuwa wao waliingia kwenye TANU wakati Rais akiwa
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, walipata fursa ya kukaa pamoja na
kuzungunza juu ya mambo mbalimbali yakiwamo ya chama pamoja na maendeleo
ya Watanzania kwa ujumla.
Akindole alisema sababu kubwa iliyomfanya kuhamia CHADEMA ni kuona uongozi wa CCM wa sasa ukiwanyanyasa wananchi kupita kiasi na kunyamazishwa pindi wanapokuwa na maneno ya kushauriana juu ya maendeleo ya kijiji chao. “Kwa sababu hiyo mimi nimeamua kutoka kwenye Chama cha CCM na kuhamia CHADEMA ili nijaribu kuona msimamo unakwendaje, maana tunanyanyaswa kupita kiasi na tukitaka kulalamika serikali haitusikilizi, na mbunge akija hapa tukilalamika hata yeye hatusikilizi. Mimi nilikuwa na mambo yangu mengi tu nimelalamika mpaka wilayani lakini sikusikilizwa. Tufanyeje wananchi?’’ alisema Japhet.
Kwa upande wake mzee Tula amesema kuwa, wakati wa uongozi wa Mwalimu Nyerere kulikuwa na viongozi waliokuwa wamepata mafunzo ya uongozi kwa lengo la kuwasaidia wananchi lakini kwa sasa wananchi wakilalamika viongozi hawatoi msaada wowote zaidi ya kukandamizwa kutokana na viongozi wengi kukosa maadili ya uongozi. “Hapa nilipo nina miaka 75, mzee kama mimi sikuwa na haja ya kuhama hama chama, lakini ninatafuta msaada, kama CCM kungekuwa na msaada viongozi wasio bora wangekuwa wanaonywa na kufuata maadili ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwa kweli nisingehama,“ alisema Tula.
Aidha, wazee hao wamesema kuwa, licha ya wao kuhamia CHADEMA, lakini bado wanaiomba serikali kumchukulia hatua mwenyekiti huyo wa Kijiji cha Kihesa Mgagao ambaye pia ni diwani wa kata na mwenyekiti wa CCM, kwani hawatendei haki wazee wa kijiji hicho na wananchi kwa ujumla na uongozi wake ni wa kidikteta.
CHADEMA yaiburuza CCM Uchaguzi Geita
Huko Chato, katika Mkoa mpya wa Geita, CHADEMA kimepata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa wenyeviti wa serikali za vijiji baada ya kuibwaga CCM kwa kupata vijiji vinane kati ya 11 vilivyokuwa vikishindaniwa. Uchaguzi huo mdogo wa kuziba nafasi zilizoachwa wazi na baadhi ya viongozi waliokuwepo awali jimboni humo kutokana na sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vifo ambao ulifanyika hivi karibuni uliwafanya baadhi ya Wana CCM kujiunga na CHADEMA mara baada ya matokoeo kutangazwa akiwamo aliyekuwa mgombea wa CCM wa Kijiji cha Minkoto.
Nafasi zilizogombewa zilikuwa zikishikiliwa na viongozi wa CCM kabla ya baadhi yao kujiuzulu, kuhamia vyama pinzani na wengine kuhama makazi yao na kwenda maeneo mengine. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, msimamizi msaidizi wa uchaguzi huo, Sodio Nyuga alisema CHADEMA kimefanikiwa kutwaa nafasi 8 za vijiji dhidi ya tatu zilizonyakuliwa na CCM . Hata hivyo, CCM ilijifariji kwa kutwaa uenyekiti katika vitongoji 28 na CHADEMA kikipata nafasi 10, wakati wajumbe wa serikali za mitaa CCM kilijipatia wajumbe 92 na CHADEMA 46.
Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Chato, Mange Sai, alisema ushindi uliopatikana ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa wilaya hiyo kwa kuwa baadhi ya vitongoji CHADEMA ilipitisha wagombe pasipo kuwa na upinzani wa chama tawala jambo ambalo linaonyesha wazi kukubalika kwa chama hicho kwa wananchi. Alisema kuwa CHADEMA kilitegemea kuibuka kidedea katika uchaguzi huo mdogo kutokana na wapiga kura kuchoshwa na ahadi mbalimbali za serikali ya CCM ambazo zimekuwa hazina utekelezaji na badala yake baadhi ya viongozi wamekuwa wakijinufaisha kwa maslahi yao binafsi huku wakiwaacha wananchi wakitaabika.
Subscribe to:
Posts (Atom)