Kufuatia uamuzi wa Spika wa Bunge jana jumamosi tarehe 28 Julai 2012
kukubali kuvunja Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini
nimetakiwa kutoa maoni yangu kuhusu uamuzi husika kwa nafasi yangu ya
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini na mbunge: Kwa maoni yangu uamuzi huo
ni sahihi lakini umechelewa na pekee hauwezi kurejesha heshima ya bunge
kwa ukamilifu wala hautaweza kushughulikia uzembe na udhaifu ulioko
kwenye bunge na kwenye serikali ikiwa hautaambana na hatua nyingine za
ziada na za haraka.Kwa upande mwingine, uamuzi huo umedhihirisha
nilichokisema kwa nyakati mbalimbali kuhusu uzembe wa kibunge pamoja na
udhaifu wa serikali.
Ukiondoa tuhuma za wabunge wanaodaiwa
kupokea rushwa ama kuwa na maslahi ya kifedha kwenye wizara, taasisi au
mashirika wanayoyasimamia kwenye kamati mbalimbali, heshima ya bunge
imeathiriwa vile vile na maamuzi mathalani uamuzi wa kuchaguliwa kwa
mtuhumiwa wa ufisadi wa Rada Mbunge Andrew Chenge kuwa mwenyekiti wa
Kamati ya Fedha na Uchumi.
Hivyo hatua zaidi zichukuliwe ikiwa
ni pamoja na kuvunja na kamati zenye wajumbe waliotuhumiwa na pia
kufanya mabadiliko makubwa kwenye wajumbe wa kamati mbalimbali za kudumu
za bunge ili kupunguza maslahi ya kifedha ama tuhuma za rushwa miongoni
mwa wajumbe wa kamati. Aidha Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya
Bunge imalize kazi yake kwa dharura ili majina ya wahusika yatajwe ndani
ya bunge na bunge lijadili kupitisha maazimio ya hatua za ziada za
kuchukuliwa na vyombo huru vya kiuchunguzi na hatimaye watakaothibitika
kuvunja sheria wafikishwe mahakamani. Pamoja na hatua hizo, Kamati za
Vyama nazo zichukue hatua kwa wabunge wake watakaotajwa ili kudumisha
misingi ya uadilifu na uwajibikaji kwa maslahi ya umma.
Hata baada ya
hatua hizo, izingatiwe kuwa Bunge litaweza kujinasua kwenye uzembe
ikiwa litatimiza kikamilifu wajibu wake wa kuisimamia serikali kwa
mujibu wa ibara ya 63 kuondoa udhaifu wa serikali kwenye sekta ya
nishati na sekta nyingine muhimu za taifa kwa kuhakikisha maazimio yote
ya bunge yanatekelezwa kwa ukamilifu na kwa haraka kama nilivyoeleza
kwenye maoni ya kambi rasmi ya upinzani bungeni tarehe 15 Julai 2011 na
tarehe 27 Julai 2012.
Nilisema bungeni kwamba “Naamini iwapo
maazimio ya Bunge juu ya Mkataba baina ya TANESCO na Kampuni ya Richmond
Development Company LLC yangetekelezwa yote na kwa wakati toka mwaka
2008, maazimio ya bunge juu ya uendeshaji wa sekta ndogo ya gesi asili
ya mwaka 2011 yangezingatiwa yote na kwa haraka, maazimio kuhusu uhalali
wa utaratibu wa Wizara ya Nishati na Madini kuchangisha fedha kwa ajili
ya kupitisha bajeti bungeni ya mwaka 2011 yangechukuliwa kwa uzito
unaostahili; taifa lingeepushwa kurudia mijadala ile ile kuhusu Wizara
hii hii mara kwa mara”.
Mathalani, Waziri wa Nishati na Madini
ameeleza bungeni tarehe 28 Julai 2012 kuwa wapo wabunge wanaotuhumiwa
kufanya biashara zenye kulihujumu Shirika la Umeme (TANESCO) na Spika wa
Bunge akahitimisha kuwa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge
itachunguza tuhuma husika na pia kwamba inakusudiwa kutungwa kwa Kanuni
za Maadili (Code of Conduct) ili kudhibiti hali hiyo.
Hata hivyo,
Serikali na Uongozi wa Bunge kwa pamoja wamesahau kuwa mwaka 2008 baada
ya Kashfa ya Richmond iliazimiwa katika Azimio Na. 11, kwamba “Sheria
ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya Mwaka 1995 (The Public Leadership Code
of Ethics Act), ifanyiwe marekebisho makubwa ili kudhibiti utaratibu
unaoonekana wa kawaida sasa wa Viongozi Waandamizi wenye dhamana ya
kisiasa kuendelea na biashara zao binafsi wakiwa madarakani, jambo
ambalo lina mgongano wa kimaslahi. Serikali ianze rasmi maandalizi ya
majadiliano ya kina kuhusu suala hili ndani na nje ya Bunge kwa
kuwashirikisha wadau mbalimbali.”
Bunge lilitaarifiwa Februari
2010 kuhusu utekelezaji wa Serikali kwamba kikundi kazi (Task Force)
kiliundwa ambacho kiliandaa waraka wenye mapendekezo ya kurekebisha
Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, (Sura 398) ambao ulikuwa katika
ngazi ya kujadiliwa na Kamati ya Makatibu Wakuu (IMTC). Aidha, Bunge
lilielezwa kuwa serikali ilitarajia kuwasilisha muswada husika katika
mkutano wa kumi na tisa wa Bunge la tisa. Muswada huo haukupitishwa
katika Bunge la tisa kama ilivyoshauriwa na kamati na mpaka kutokana na
uzembe na udhaifu azimio hilo halijatekelezwa na tuhuma nyingine
zimeendelea kuibuka.
Aidha, kumetolewa madai ya baadhi ya wabunge
kupokea ama kudai rushwa suala ambalo nalo Spika wa Bunge ametoa uamuzi
kuwa litashughulikiwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.
Lakini Serikali na Uongozi wa Bunge kwa pamoja wamesahau kwamba hii si
mara ya kwanza kwa tuhuma za namna hiyo kutolewa juu ya baadhi ya
wabunge wa kamati mbalimbali za bunge.
Hata hivyo, kwa sababu ya
kutochukua hatua kwa haraka na kwa ukamilifu tuhuma kama hizo
zitaendelea kujirudia hata baada ya kuvunjwa kwa kamati ya bunge ya
nishati na madini. Izingatiwe kwamba madai ya rushwa kutolewa kwa
wabunge yaliwahi kujitokeza kuhusu Kamati ya Nishati na Madini na
binafsi nilitoa ushuhuda kwa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG) mwaka 2011, na nikatoa ushuhuda tena kwa Kamati Teule ya Bunge
iliyochunguza uhalali wa utaratibu wa Wizara ya Nishati na Madini
kuchangisha fedha kwa ajili ya kupitisha bajeti bungeni mwaka 2011 kuwa
yamekuwepo matukio ya kushawishi wabunge kwa rushwa hata hivyo hatua
hazikuchukuliwa ama kuvunja kamati zilizotajwa au kuwachukulia hatua
wahusika.
Suala hili likatajwa tena na Mbunge wa Kigoma
Kaskazini David Kafulila kuhusu Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa na
likatajwa tena na Kiongozi wa Upinzani Freeman Mbowe na Mbunge wa Kyela
Dr Harrison Mwakyembe kuhusu uchaguzi wa Afrika Mashariki lakini hatua
hazikuchukuliwa kuchunguza wabunge husika na kuchukua hatua. Iwapo
maazimio kuhusu uhalali wa utaratibu wa Wizara ya Nishati na Madini
kuchangisha fedha kwa ajili ya kupitisha bajeti bungeni ya mwaka 2011
(Maarufu kama Sakata la Jairo), yangetekelezwa na wahusika
wangechukuliwa hatua ingejenga nidhamu pia kwa watendaji wa wizara na
mashirika ya umma kuhusu rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma
yenye kulenga kuwaathiri wabunge kwa rushwa na maslahi mengine ya
kifedha.
Katika hali inayoonyeha kwamba Serikali bado haioni
uharaka na ulazima wa kuchukua hatua, wakati bunge lilipokaa kama kamati
tarehe 28 Julai 2012 kupitisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini
nilitaka ufafanuzi kutoka kwa Waziri wa Nishati na Madini kuhusu
utekelezaji wa maazimio hayo ambayo mpaka sasa hakuna taarifa ya
utekelezaji iliyowasilishwa bungeni toka yapitishwe mwezi Novemba mwaka
2011; lakini Waziri akajibu tu kwamba hawezi kufanyia kazi taarifa za
magazetini, bila kujali kwamba nilichouliza hakihusu taarifa za
magazetini bali maazimio ya bunge baada ya kazi iliyofanywa na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali na ikarudiwa tena na Kamati Teule ya Bunge
ambayo ilihoji wahusika na kupata pia vielelezo.
Kwa hiyo, ni
muhimu Serikali na Uongozi wa Bunge ukarejea kwenye Hotuba
niliyowasilisha bungeni na kuchukua hatua kwa usimamizi wa Rais, Waziri
Mkuu na Spika wa Bunge juu ya masuala yote niliyoyaeleza. Pamoja na
kutaja ushawishi uliokuwa ukifanywa kwa wabunge kuhusu suala la ununuzi
wa mafuta ya IPTL, na ufisadi ndani ya TANESCO nilieleza pia masuala
mengine makubwa kwenye nishati na madini yenye kuhusu mabilioni ya
shilingi kwenye mikataba mikubwa ya umeme, madini, mafuta na gesi asili
pamoja na hatua za mabadiliko ya kimfumo zinazopaswa kuchukuliwa.
Nimetoa maoni haya leo, Jumapili tarehe 29 Julai 2012:
John Mnyika (Mb)
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini
SERIKALI ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, imelifungia gazeti la MwanaHalisi kwa muda
usiojulikana kwa kile kilichoelezwa kuwa na mwenendo wa kuandika habari
na makala za uchozezi.
Sababu nyingine ya kufungiwa kwa gazeti hilo ni pamoja na kujenga uhasama na uzushi likiwa na nia ya kusababisha wananchi kukosa imani na vyombo vya dola hali inayoweza kuhatarisha amani na mshikamano wa nchi.
Akisoma tamko la Serikali leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Wizara ya Habari (MAELEZO), Phabian Lugaikamu, alisema kuwa katika toleo la gazeti hilo namba 302, 303 na 304 ya mwaka 2012 na mengine yaliyotangulia yalichapisha habari na makala zenye kueneza na kujenga hofu kwa jamii. '
“Mhariri wa gazeti la Mwanahalisi ameitwa na kuonywa mara nyingi lakini hataki kukiri kuwa maudhui ya makala zake hazina tija kwa jamii,pia hazifuati weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari” alisema.
Aidha, alisema kuwa mhariri huyo mara zote katika utetezi wake amekuwa akinukuu kifungu cha 18 cha katiba ya nchi kinachotoa uhuru wa kutoa maoni na kwa makusudi kutokunukuu kifungu ca 30 cha katiba hiyo kinachoweka ukomo wa uhuru.
“Serikali imeamua kulifungia gazeti hilo kutochapishwa kwa muda usiojulika kwa mujibu wa sheria ya magazeti ya mwaka 1976, kifungu namba 25(i), adhabu hiyo itaanza tarehe 30 Julai, 2012 kwa mujibu wa tangazo la serikali namba 258 lililochapishwa katika gazeti la Serikali na kutolewa jijini Dra es Salaam Julai 27, 2012” alisema.
---
habari via Francis Dande/Habari Msego blog
Sababu nyingine ya kufungiwa kwa gazeti hilo ni pamoja na kujenga uhasama na uzushi likiwa na nia ya kusababisha wananchi kukosa imani na vyombo vya dola hali inayoweza kuhatarisha amani na mshikamano wa nchi.
Akisoma tamko la Serikali leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Wizara ya Habari (MAELEZO), Phabian Lugaikamu, alisema kuwa katika toleo la gazeti hilo namba 302, 303 na 304 ya mwaka 2012 na mengine yaliyotangulia yalichapisha habari na makala zenye kueneza na kujenga hofu kwa jamii. '
“Mhariri wa gazeti la Mwanahalisi ameitwa na kuonywa mara nyingi lakini hataki kukiri kuwa maudhui ya makala zake hazina tija kwa jamii,pia hazifuati weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari” alisema.
Aidha, alisema kuwa mhariri huyo mara zote katika utetezi wake amekuwa akinukuu kifungu cha 18 cha katiba ya nchi kinachotoa uhuru wa kutoa maoni na kwa makusudi kutokunukuu kifungu ca 30 cha katiba hiyo kinachoweka ukomo wa uhuru.
“Serikali imeamua kulifungia gazeti hilo kutochapishwa kwa muda usiojulika kwa mujibu wa sheria ya magazeti ya mwaka 1976, kifungu namba 25(i), adhabu hiyo itaanza tarehe 30 Julai, 2012 kwa mujibu wa tangazo la serikali namba 258 lililochapishwa katika gazeti la Serikali na kutolewa jijini Dra es Salaam Julai 27, 2012” alisema.
---
habari via Francis Dande/Habari Msego blog
TAMKO LA SERIKALI LA KULIFUNGIA GAZETI LA MWANAHALISI
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelifungia kutochapishwa gazeti la MwanaHalisi kuanzia 30 Julai, 2012 kwa muda usiojulikana kutokana na mwenendo wake wa kuandika habari na makala za uchochezi, uhasama na uzushi likiwa na nia ya kusababisha wananchi kukosa imani na vyombo vya dola hali inayoweza kuhatarisha amani na mshikamano uliopo nchini.
Katika matoleo yake hivi karibuni, gazeti la MwanaHalisi toleo Na. 302 la Jumatano Julai, 11 – 18, 2012 na toleo Na. 303 la Jumatano Julai 18 – 24, 2012 na toleo Na. 304 la Jumatano Julai 25 hadi 01 Agosti, 2012 na mengine yaliyotangulia yamekuwa yakichapisha habari na makala zenye kueneza na kujenga hofu kwa jamii. Mhariri wa gazeti la MwanaHalisi, ameitwa na kuonywa mara nyingi, lakini hataki kukiri kuwa maudhui ya makala zake hazina tija kwa jamii, pia hazifuati weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.
Mhariri, mara zote katika utetezi wake amekuwa akinukuu kifungu cha 18 cha Katiba ya nchi yetu ambacho kinatoa uhuru wa kutoa maoni na kwa makusudi kutonukuu kifungu cha 30 cha Katiba hiyo kinachoweka ukomo wa uhuru.
Uamuzi wa Serikali
Serikali imeamua kulifungia kutochapishwa kwa muda usiojulikana gazeti la MwanaHalisi, kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, kifungu Na. (25) (i), adhabu hiyo itaanza tarehe 30 Julai, 2012 kwa mujibu wa Tangazo la Serikali (Government Notice) Na. 258 lililochapishwa katika Gazeti la Serikali na kutolewa jijini Dar Es Salaam tarehe 27 Julai, 2012.
Serikali inawataka wamiliki, wahariri na wanahabari kuzingatia sheria, uzalendo, weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari katika kutekeleza wajibu wa kuhabarisha, kuelimisha na kutoa burudani kwa wananchi.
Kama ilivyoelezwa Bungeni wakati wa kuwasilisha Bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hivi karibuni waandishi na watangazaji wa habari wanatakiwa kuhakikisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoandaa vinazingatia taaluma na kuweka mbele maslahi ya Taifa letu na uzalendo. Uhuru na haki ya vyombo vya habari uendane na wajibu.
Kuanzia sasa Serikali haitasita kuchukua hatua dhidi ya vyombo vya habari ambavyo kwa maksudi vitatoa taarifa za uchochezi ambazo zitahatarisha hali ya amani na utulivu uliopo nchini mwetu.
Imetolewa na OFISI YA MSAJILI WA MAGAZETI
WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
30 Julai, 2012











.



