Thursday, April 26, 2012

WAZIRI WA UCHUKUZI OMARY NUNDU AMESEMA HANA KOSA BADO ANATAFAKARI

Press Co imekwisha Waziri Nundu kashuka na hoja 10 za nguvu zifuatazo.

1. Ujenzi wa Gati No 12 na 14.
TPA wanaipigia chapuo kampuni CCC ya Uchina kujenga kwa gharama za mkopo wa dola appx 600 toka Exim Bank ya China. Waziri Nundu amekiri kuingilia kati sio mpaka sebulen bali hadi chooni kwenye uchafu wenyewe!.

Hiyo kampuni ya CCC ilipatikanaje?.
Waliofanya feasibility study ni hao hao CCC wanaotaka kujenga ni hao hao CCC na mkopo walioomba toka benki ya Exim ya China ni hao hao CCC. Waziri amepinga kwa kutaka ushindani wa wazi!. Wenzetu Mombasa wamejenga gati kama hizo kwa less than 200 millions, kwa nini sisi tujenge kwa dola milioni 600 tena bila ushindani wa wazi, why?.

2.2. Baada ya kuona waziri anawakwamisha CCC wakaamua kuyapitishia madudu yao kwa Naibu waziri. wakampa paid trips kutembelea miradi mbalimbali ya CCC duniani pote, Naibu waziri yeye hana bei, akaingia kichwa kichwa kuwa kuwadi wao. Alianza kupigwa trips za nje ya nchi bila kibali cha waziri wake, kwa lugha nyingine ni uwezekano wa Ikulu kuhusika kwa Naibu Waziri huyo kusafiri nje ya nchi bila waziri kujua. Mazingira ya safari hizo za naibu waziri zina viashiria vyote vya rushwa ya "free bees" under pretex ya "facility visit" under transparency lazima Naibu Waziri aseme amelipwa shin ngapi amesafirishwa tiketi za ndege za daraja gani na alifikia hoteli za nyota ngapi?.

Wachini huwa hawasafiri 1st Class, hawalipani per diem nono wala hawakai hoteli ya nyota 5!, ila makampuni yamayo sololea tenda, huwalipa maofisa wa nchi per diem nene, kuwasafirisha kwa 1st class na kuwalaza hoteli za nyota 5!.

No comments:

Post a Comment