Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeunda Mkoa
Maalum wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu na kufanya uteuzi wa makatibu tisa
wa mikoa.
Makatibu walioteuliwa na mikoa yao kwenye mabano ni pamoja na;-
Makatibu walioteuliwa na mikoa yao kwenye mabano ni pamoja na;-
1. Ndg. Elikana Mauma (Mkoa wa Mara)
2. Ndg. Hilda Kapaya (Mkoa wa Geita)
3. Ndg. Shaibu Akwilombe (Mkoa wa Simiyu)
4. Ndg. Hosea Mpagike (Mkoa wa Njombe)
5. Ndg. Alphonce Kinamhala (Mkoa wa Katavi)
6. Ndg. Aziza R. Mapuri (Mkoa wa Magharibi)
7. Ndg. Maganga Sengerema (Atapangiwa kituo)
8. Ndg. Adelina Geffi (Atapangiwa kituo)
9. Ndg. Christopher Ngubiagai (Mkoa Maalum wa Wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu)
Kuundwa kwa mkoa maalum wa wanafunzi wa elimu ya juu kunalenga kupanua
wigo ikiwa ni mkakati wa chama kujiimarisha zaidi kwa wanachama wake wa
kada mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa elimu ya juu.
Uamuzi
huu utawapa fursa wanafunzi wasomi ambao wengi wao ni vijana kupata
fursa za kikatiba na kanuni kushauri na kushiriki moja kwa moja katika
maamuzi ya ngazi ya juu katika chama cha Mapinduzi (CCM).
Nape M. Nnauye
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM
Itikadi na Uenezi
Source:www.ccmchama.blogspot.com
No comments:
Post a Comment