MADAI
MAKUBALIANO
HALI ILIVYO SASA
- HOSPITALINI: hakuna huduma za afya (matibabu, upimaji wala upasuaji), YAANI NI KWELI TUMEGOMA
- VYOMBO VYA HABARI: Kuna upotoshwaji mkubwa wa taarifa kwa umma.
- MTAANI: Hofu na mashaka kwa wananchi kutokana na kutoelewa matamko yanayopingana kati ya Serikali na Tamko la madaktari
MTAZAMO
HEBU ANGALIA KATIKA MAKUBALIANO NI LIPI LIMETEKELEZWA HADI SASA?? THEN SERIKALI INAONGEZA MISHAHARA YA WABUNGE, HIVI KARIBUNI UTASIKIA SABASABA!!!
- Jumla ya madaktari wote ni chini ya 15,000 (na hapa namaanisha General practitioners and Specialists). Kwa uchache au wingi wetu tumekwisha kuona madhara ya migomo miwili iliyokwishatokea.Nashangwazwa na kuona baadhi ya watu wanaosema madaktari hatuna utu wala huruma na tunaweka maslahi yetu mbele, hivi mnajua kuwa katika nchi za East and Central Africa, Tanzania ndiyo yenye kulipa mishahara midogo kwa watu wa sekta ya Afya?? Rwanda juzi juzi (1994) walikuwa na vita lakini daktari analipwa 1500USD, au mnadhani hatujui kuna nchi za jirani na mbali tunaweza kwenda kama wenzetu (Mf. Rwanda, Botswana, Zambia, Lesotho, Egypt, SA, nk) ??? mnadhani kubaki kwetu Tanzania tuteseke kwa kauli eti “UDAKTARI NI WITO?”, “WATANZANIA -WATOTO, KINA MAMA, NA WAZEE WATAKUFA IWAPO TUKIGOMA”, “OOOH?? HATUTAKIWI KUGOMA”…tumeonyesha uzalendo wetu kwa kubaki hapa hapa na mazingira yetu magumu, lakini sasa IMEFIKA MWISHO.
Pediatrics(wodi ya watoto):Hakuna vifaa vya kuongezea maji/damu mwilini(cannula), hakuna mitungi ya gesi, OBGYN(wodi ya kina mama);hakuna pamba, mipira ya mikojo(urine bags), MOI, Mwaisela hakuna vitanda, Operating Theatre,OT; Hakuna gloves ,mask, kofia za kutosha, Huduma ya mionzi ya CT SCAN ni mwezi wa saba haifanyi kazi(huku mmiliki akiwa anaidai Wizara ya Afya mil.800/=Tsh)na haitakuwepo hadi atakapolipwa.
Kwa madai hayo, si lazima serikali itekeleze all at once, lakini Mshahara unazungumzika, wale mnaofanya interview, huwa hamuulizwi ni kiasi gani unategemea kuanza nacho na waajiri wenu? Doesn’t this make salary being negotiable?? Then kwanini isiwe kwetu?
Hivi ulishawahi kusikia MASS RESIGNATION????? It takes ATLEAST 12yrs kumpata huyo specialist after elimu ya sekondari, Halafu nasikia mnasema eti tufukuzwe kazi?Then what??? Kwa wale wenye mtazamo mfupi mnadhani Serikali inaweza ku-import madaktari toka nje.
Kwa mfano:
Then NASIKIA MTATUPELEKA MAHAKAMANI.
Utawakamata madaktari wote nchini?? Kumbuka huu mgomo hauna kikomo na hauna kiongozi!!!..hypothetically speaking ukitupeleka, tutawatibu tukiwa huko gerezani?? Waliobaki mnadhani watarudi makazini?tukirudi mnadhani tutafanya kazi? Tukifanya kazi unadhani itakuwa katika kiwango kinachotakiwa? With demoralization unategemea tutaponyesha ndugu zetu kweli, au mortality kuwa juu??? Then kwa wanafunzi walio vyuo vya tiba kama MUHAS, WBUCHS, KCMC, UDOM, HKMU, IMTU..watafanya kazi hapa nchini kwa hali hii, ama Brain drain ndiyo itazidi!!
SIASA
Wananchi walishazoea kudanganywa, na hii imezoeleka na viongozi Fulani kushindwa kufanya wajibu wao kusingizia wanasiasa kadhaa..Hapa HAKUNA siasa ila mkiileta tutawaachia tu kwani huko hatupawezi ila viongozi mjue hakuna tena rufaa ya kwenda nje (mf. INDIA) MUHIMBILI
Hivi wananchi mnajua viongozi wanalipwa kiasi gani wanapoenda nje kutibiwa na familia???
Eti kwa sababu sekta nyingine hawawezi kugoma, ndio na sisi tusigome? Eti kwa sababu askari anayetumia SMG na kupambana na jambazi anayetumia AK47, eti kwa sababu mishahara ya walimu inacheleweshwa, ndio tusigome??? Nani kasema??
HITIMISHO
HAPA KAZINI HATURUDI…HII IELEWEKE VIZURI…HATURUDI….MGOJA NIIWEKE VIZURI HATURUDI, ACHA MEDIA IENDELEE KUDANGANYA, LAKINI UKWELI TUNAUJUA, MWISHONI MTARUDI TU, NA THIS TIME SI TENA YA KUTUMIA BUSARA ZETU KUWASTAHI VIONGOZI NA KISHA KWENDA PALE KUONGEA NA ‘WAZEE WA DSM”
“Doctors we might be slow walkers, but we never walk back” Solidarity Forever!
from wavuti.com
No comments:
Post a Comment