Aliyekuwa mgombea Ubunge wa jimbo la Ubungo, Dar es Salam kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, CCM, mwaka 2010 Hawa Ng'umbi leo amewasilisha hati ya nia ya kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa.
Kusudio hilo limewasilishwa leo na wakili wake Mh. Issa Maige baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutupilia mbali kesi aliyoifungua awali kupinga ushindi wa kiti cha Ubunge alioupata Mhe. John Mnyika (Chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA) mwezi uliopita.
Hukumu ya kesi hiyo ilithibitisha ushindi wa Mnyika
Source: http://www.wavuti.com
No comments:
Post a Comment