Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amewateua Majaji 10 wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuanzia jana
Alhamisi, Juni 7, 2012.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Y Sefue jioni ya leo, Ijumaa,
Juni 8, 2012, walioteuliwa ni Ndugu Francis Sales Katabazi Mutungi,
Ndugu Sam Mpaya Rumanyika, Ndugu Patricia Saleh Fikrini, Dkt. Gerald
Alex Mbonimpa Ndika na Ndugu Salvatory Benedict Bongole.
Wengine
walioteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania ni Ndugu Mathew
Pauwa Mhina Mwaimu, Ndugu Jacob C.M. Mwambegele, Ndugu Latifa Mansoor,
Ndugu John Samwel Mgetta na Ndugu Joaquine Antoinette De-Mello.
Kabla
ya uteuzi wake Ndugu Mtungi alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani
Tanzania, Ndugu Rumanyika alikuwa Msajili wa Baraza la Rufani la Kodi,
Ndugu Fikirini alikuwa Hakimu Mkazi Mkuu, Ndugu Ndika alikuwa Mkuu wa
Chuo cha Sheria Tanzania na Ndugu Bongole alikuwa Naibu Msajili
Mwandamizi, Mahakama Kuu.
Ndugu Mwaimu alikuwa Mkurugenzi wa
Idara ya Katiba na Haki za Binadamu, Ndugu Mwambegele alikuwa Msaidizi
wa Katibu wa Baraza la Mawaziri, Ndugu Mansoor alikuwa Wakili katika
Latifa Law Chambers, Ndugu Mgetta alikuwa Hakimu Mkazi Mkuu na Naibu
Msajili wa Mahakama ya Rufani na Ndugu De-Mello alikuwa Wakili wa
Kujitegemea.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment