Binti wa kidato cha pili
katika Shule ya Sekondari Tongani, katika kata ya Mkaramo, wilayani
Pangani (jina linahifadhiwa) ametoroka kwao na kukimbilia kwa Mkuu wa
Wilaya ya Handeni kuomba msaada, akikwepa kuachishwa shule na
kufungishwa ndoa kwa nguvu na babu yake.
Binti huyo mwenye umri wa miaka 15 ambaye ni mkazi wa kitongoji cha Mbugani katika kijiji cha Mkaramo, wilayani humo, alilazimika kukimbia kwao na kwenda kulala kichakani baada ya kulazimishwa kuacha shule ili aolewe wakati mwenyewe anataka kutimiza ndoto zake za kuendelee na masomo.
Akizungumza na NIPASHE jana akiwa katika eneo la ofisi za mkuu wa wilaya ya mjini Handeni, Binti huyo alisema kwamba tukio hilo lilitokea juzi majira ya mchana kijijini hapo, kufuatia babu yake kutaka kumchapa viboko kumlazimisha aolewe.
Alieleza kwamba, aliamua kuchukua uamuzi huo mgumu baada ya kuona akifikisha suala hilo kwa serikali ya wilaya hiyo ambayo amesikia ina mradi wa kukomboa wasicha unaoitwa ‘Niache Nisome’ atasaidiwa ili aweze kusoma.
Agnes ambaye ni mmoja kati ya watoto wanne wa familia yao ndiye pekee anayesoma na alieleza kwamba wazazi wake wote walifariki dunia miaka mingi, ambapo mama yake alifia mkoani Dodoma.

Mimi ninaishi kwa Babu yangu huko Mbugani Mkaramo, alitaka kuniozesha mwanaume ambaye wala sijawahi kumuona, lakini nadhani naye ni Mmang’ati. Alitaka niache shule ili niolewe, nikamkatalia kwavile nataka nisome, alivyoona vile alitaka kunipiga...
Niliamua kukimbilia kujificha porini majira ya saa 5:00 asubuhi hadi saa 10 usiku, nikapanda gari ya kwenda Mkata, nilipofika huko nikapata gari nyingine iliyonifikisha kwa Mkuu wa Wilaya. Lengo langu ni kuomba msaada serikali inisaidie nisome au ikibidi niweze kufika kwa ndugu zangu Dodoma ili nisome.
Sijui mwenyewe alitaka kupewa mahari kiasi gani, maana kuna aina mbili ya mahari katika kabila letu. Kuna ng’ombe watatu na debe tatu za asali, nyingine ni ng’ombe saba, labda alitaka apate mali.
Pia, huku nimesikia serikali inawasaidia wasichana ili wasome kwa kuvunja ndoa za wanafunzi.
Akizungumzia
tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alisema
kwamba anaona faraja kubwa mafaniko yanayopatikana katika mradi wa
Niache Nisome ambao umeanzishwa kwa ajili ya kumkomboa mtoto wa kike
dhidi ya mimba na ndoa za utotoni.
Huyu mtoto amenishangaza sana, ameonyesha ujasiri wa ajabu kwenda kulala porini ni jambo la ujasiri wa hali ya juu. Pia, nimeshangaa kwa mabinti sasa kutambua kwamba Serikali yao inawajali katika elimu kwa kuwatetea ili wafikie malengo yao...
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani Handeni, Athumani Malunda, pamoja
na Katibu wake Salehe Kikweo ambao walishuhudia tukio hilo,
walimpongeza binti huyo kwa ujasiri aliouonesha katika msimamo wake wa
kutaka kusoma.
No comments:
Post a Comment