WABUNGE wa upinzani jana walizua tafrani bungeni na
kusababisha kikao kilichokuwa kikiongozwa na Naibu Spika, Job Ndugai
kuvu njika kabla ya muda uliokuwa umepangwa. Wabunge hao wa upinzani
walisimama wote kwa pamoja na kuanza kupiga kelele za kupinga hatua ya
Ndugai kuruhusu kujadiliwa kwa hoja ya Waziri wa Maji, Profesa Jumanne
Maghembe.
Profesa Maghembe katika hoja yake ambayo iliungwa mkono na wabunge wa
CCM, alikuwa akipendekeza kuo ndolewa bungeni kwa hoja binafsi
iliyokuwa imewasilishwa mapema na Mbunge Ubungo (Chadema), John Mnyika.
Mnyika katika hoja yake alikuwa akitaka Bunge lia zimie kuitaka
Serikali ichukue hatua za haraka ya kuboresha upatikanaji wa majisafi na
ushughulikiaji wa majitaka katika Jiji la Dar es Salaam.
Baada ya Ndugai kuruhusu hoja ya Profesa Maghembe kujadiliwa badala
ya hoja ya Mnyika, wabunge wa upi nzani walisimama na kuanza kupiga
kelele za kupinga kile walichodai kwamba ni Naibu Spika kuvunja kanuni
ambazo anapaswa kuzisimamia.
Ilivyokuwa
Profesa Maghembe aliyekuwa mchangiaji wa kwa nza katika hoja ya Mnyika
alitoa kauli kwamba Serikali inaendelea kukamilisha miradi mbalimbali ya
maji jijini Dar es Salaam, hivyo kutaka hoja ya Mnyika iondolewe.
Kabla ya kutamka maneno hayo, tayari wabunge wa upinzani bila kujali
vyama vyao walikuwa wameanza kumzomea na kupiga kelele kiasi kwamba
maneno yake ya mwisho hayakusikika.
Baada ya hapo alisimama Naibu Spika na kuwataka wabunge watulie ili
waanze kuchangia hoja hiyo na alimtaka Mnyika kuzungumza, lakini kabla
ya Mnyika, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee alisemama na kuanza kuzungumza
baada ya Naibu Spika kumruhusu.
“Mheshimiwa Naibu Spika naona mwendelezo wa uvunjwaji wa taratibu na
kanuni za Bunge, hoja binafsi zinaratibiwa na kanuni ya 57 na
58,”alisema Mdee na kuongeza;
“Kanuni hizi mbili ukizisomaoi Waziri anatakiwa kueleza kipengele gani kitoke…….”
Kabla Mdee hajamaliza kueleza Naibu Spika, alisimama na kumtaka
Mnyika achangie kama alikuwa ana la kusema, lakini akamkatisha na kelele
zikaanza bungeni.
Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani, Tundu Lissu alisimama kutaka utaratibu,
lakini Naibu Spika Ndugai alimkatisha kisha akasema “Waswahili wanasema
kuchamba kwingi……”
“Wewe ni “Chief Whip” (Mnadhimu Mkuu) upande wa Serikali umetoa hoja
na sisi tunachangia hivyo tunachangia sasa,” alisema Naibu Spika na
kumwita Mdee aendelee kuchangia.
Hata hivyo, Mdee alikataa na Naibu Spika alimwita Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Zarina Madabida kuendelea kuchangia.

No comments:
Post a Comment