|
Hadija Jumanne SPIKA wa Bunge, Anne Makinda, amesema nchi yoyote haiwezi kuwa na maendeleo kama vijana hawatakuwa wabunifu wa kazi na kujiajiri. Akipokea mitambo mitatu ya kutengenezea barabara kwa Mkoa wa Njombe jana, Makinda alisema licha ya halmashauri yake kupokea mitambo hiyo, aliomba boza la kunyunyizia maji wakati ujenzi wa barabara. Mitambo hiyo yenye thamani ya Sh716 milioni, ilitolewa na Kampuni ya GF Truck and Equipments ya Dar es Salaam, inayojishughulisha na uuzaji mitambo mbalimbali. “Nashukuru kampuni hii kwa kutoa mitambo mitatu ila ningeomba pia watuongezee boza ili kazi ya kutengeneza barabara iwe nzuri,” alisema Makinda na kuongeza: ”Hii mitambo mitatu itatufaa hasa tukiwa na boza, kwani eneo letu ni udongo tifutifu hivyo iwapo Kampuni ya FG itaongeza kifaa hicho, ujenzi wa miundombinu utakua haraka na kubadilisha mji wa Njombe.” Awali, Ofisa masoko wa kampuni hiyo, Juma Hamsini, alisema wamefikia uamuzi wa kuikopesha kwa gharama nafuu Halmashauri ya Njombe baada ya kuwa ya kwanza nchini kuitikia wito uliotolewa na kampuni hiyo. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mji wa Njombe, George Mkindo, alisema hatua hiyo imefikiwa baada kuvutiwa na ubunifu wa hali ulionyeshwa na halmashauri yake katika upimaji viwanja na uboreshaji mji wa Njombe. |
Wednesday, May 30, 2012
Spika ahimiza vijana kujiajiri
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment